Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za
Michezo Tanzania (TASWA) Juma Pinto (katikati) akizungumza na Waandishi wa
Habari nje ya Ukumbi wa Mikutano NSSF
'Water Front', mahala unapofanyika Uchaguzi mkuu wa Rais na viongozi wa
Soka wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF).
KATIKA hali isiyo ya kawaida, Waandishi wa
Habari wamezuiwa kuripoti habari za
uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), uliofanyika katika Ukumbi
wa mikutano wa NSSF Water Front.
Baada ya waandishi kuzuiwa, askari waliokuwa
wakilinda usalama katika uchaguzi huo waliwataka waandishi kuondoka na kukaa
mbali na ukumbi huo huku Mwenyekiti wa
Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo (TASWA), Juma Pinto, akiwataka
waandishi kususia kuandika na kuripoti matokeo ya uchaguzi huo ikiwa ni pamoja
na kutoandika taarifa za TFF.
Pinto alisema kitendo cha TFF kupitia kwa Mwenyekiti
wa Kamati ya uchaguzi, Hamidu Mbwezeleni, kuwazuia waandishi kuripoti habari
hizo ni cha udhalilishaji kwa kuwa waandishi ndio waliokuwa mstari wa mbele
kuandika taarifa za uchaguzi huo tangu mchakato wake ulipoanza Februari mwaka
huu.
Alisema mbali na kutoruhusiwa kuripoti uchaguzi huo,
Mbwezeleni ametoa kauli ambazo si za kiungwana na kusahau kuwa waandishi ndio
waliokuwa mstari wa mbele kuwajuza Watanzania kuhusu uchaguzi huo kwa faida ya
maendeleo ya soka la Tanzania.
Kufuatia hali hiyo, iliwalazimu waandishi kukaa nje ya ukumbi huku wakiuliza kwa wajumbe kitu gani kinachoendelea ndani ya ukumbi.
0 comments:
Chapisha Maoni