YANGA KIBOKO WAWATIMUA AZAM TV UWANJANI, ULINZI BAB KUBWA



Afisa wa Usalama (mwenye suti) akiangalia usalama katika moja la lango ya kuingia kwenye Uwanja wa Taifa.

Viongozi wa Azam TV wakiteta jambo na Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura baada ya kuzuiwa kurusha live mchezo huo.
UONGOZI wa klabu ya Yanga umewatimua wapiga picha wa Azam TV kabla ya mpira kuanza wakiwakataza wasirushe mchezo wao dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Yanga walikataa kurusha mchezo huo kwa madai kuwa mazungumzo yao kati ya klabu yao na Azam TV na Waziri wa Habari Utamaduni na Michezo.
Lakini baada ya kufanyika kwa mazungumzo kati ya pande hizo mbili wapiga picha wa Azam walionekana kurudisha kamera zao uwanjani tayari kwa kurusha katika kipindi cha mchezo huo.
Hadi mapumziko tayari Yanga walikuwa wanaongoza kwa mabao 2-0, yaliyofungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 6 na Didier Kavumbagu dakika ya 24.

Wafanyakazi wa Azam TV wakishangaa bila kujua la kufanya


Didier Kavumbagu akiifungia Yanga bao la pili huku kipa wa Mtibwa, Hussein Sharrif akijitahidi kuokoa bila mafanikio

Mrisho Ngassa akishangilia bao lake la kwanza kuifungia Yanga toka ajiunga na timu hiyo kwa mara ya pili
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List