MAJANGA MAPATO LIGI KUU, JKT RUVU NA COASTAL ZAINGIZA LAKI 2, KILA KLABU YAPATA ELFU 39MECHI ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya wenyeji JKT Ruvu na Coastal Union ya Tanga iliyochezwa juzi (Novemba 6 mwaka huu) Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam imeingiza sh. 201,000.
JKT Ruvu iliibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi hiyo namba 85 na kushuhudiwa na watazamaji 67 waliokata tiketi kwa viingilio vya sh. 3,000 na 10,000.
Kila klabu ilipata mgawo wa sh. 39,010 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 30,661.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 19,835, tiketi sh. 38,100, gharama za mechi sh. 11,901, Bodi ya Ligi sh. 11,901, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 5,950 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 4,628.
Nayo mechi kati ya Ashanti United na Simba iliyochezwa juzi Uwanja wa Taifa imeingiza sh. 24,931,000 ambapo kila klabu ilipata mgawo wa sh. 5,333,590.

Wakati huo huo, mechi za jana (Novemba 7 mwaka huu) kati ya Yanga na Oljoro imeingiza sh. 34,902,000 kutokana na watazamaji 6,045 ambapo kila klabu imepata sh. 7,812,477.95. Mechi ya Azam na Mbeya City iliyochezwa Azam Complex yenyewe imeingiza sh. 15,973,000 kwa watazamaji 4,857 na kila klabu imepata sh. 3,953,162
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List