TANZANITE YAUA 5-1, KUTUA DAR MCHANA



TIMU ya Taifa ya wanawake chini ya miaka 20 (Tanzanite) imefuzu kucheza raundi ya pili ya michuano ya Kombe la Dunia kwa ushindi wa jumla ya mabao 15-1 baada ya leo (Novemba 9 mwaka huu) kuibugiza Msumbiji mabao 5-1.
Mabao ya Tanzanite katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Taifa wa Zimpeto jijini Maputo yalipatikana kupitia kwa Sherida Boniface alipiga matatu (hat trick) wakati mengine yalifungwa na Vumilia Maarifa na Donesia Minja.
Msafara wa Tanzanite ulioongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred utawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) kesho Jumapili (Novemba 10 mwaka huu) saa 8.30 mchana kwa ndege ya LAM.
Tanzanite inayofundishwa na Rogasian Kaijage itacheza mechi ya raundi ya pili dhidi ya Afrika Kusini. Mechi ya kwanza itachezwa jijini Dar es Salaam kati ya Desemba 6 na 8 mwaka huu wakati ile ya marudiano itafanyika Afrika Kusini kati ya Desemba 20-22 mwaka huu.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List