Andy Cole akionyesha umahiri wake katika kulisakata kabumbu alipokuwa akitoa somo kwa
wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Makongo ya jijini Dar es salaam mara ya
mwisho alipotembelea Tanzania.
|
Na Mwandishi Wetu
MCHEZAJI wa
zamani wa klabu ya Manchester United Andy Cole anatarajia kutua jijini Dar es
Salaam Ijumaa hii, imethibishwa.
Ziara
ya Cole nchini inalenga kuwapatia uzoefu washindi wa tiketi za promosheni ya
Airtel ya 'Mimi ni Bingwa' ambao watasafiri kwenda kuangalia mechi za klabu ya
Manchester United moja kwa moja (live) katika uwanja wa Old Trafford pamoja na
kukabidhi vifaa vya mazoezi kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania ya
chini ya umri wa miaka 17.
Hii ni
ziara ya pili Tanzania kwa mchezaji Cole baada ya kutembelea Tanzania mwaka
2011 alipozindua mpango wa kutafuta vipaji wa Airtel Rising Star.
Akizungumza
na waandishi wa habari juu ya ziara hiyo, Meneja Uhusiano wa kampuni ya
mawasiliano ya Airtel Tanzania, Bw Jackson Mmbando alisema kuwa mchezaji huyo
mkubwa wa zamani wa Man U atakuwa na wakati wa kuzungumza na kushiriki mazoezi
na wachezaji wa timu ya Tanzania chini ya miaka 17, timu ambayo wengi wao ni
matunda ya mpango wa kuvumbua vipaji wa Airtel Rising Star.
"Andy
Cole ataongea na nyota hao wanaochipukia, na kuwashawishi kuongeza jitihada
zaidi katika michezo pamoja na kuwapatia mbinu za jinsi gani ya kufikia
mafanikio katika fani yao ya michezo.
"Mbali
na kuwaonyesha wachezaji hao njia ya mafanikio, mchezaji huyo mkubwa wa zamani
wa Manchester United pia atakabidhi vifaa vya mazoezi kwa timu hiyo,"
alisema Mmbando.
Alisema
kuwa Cole pia atahudhuria droo ya moja kwa moja (live) ya kuwatafuta na
kuwatangaza washindi wa tiketi tatu za kwenda Old Trafford, kabla ya kuungana
na washabiki wa Man U kuangalia mechi moja kwa moja (live) itakayoonyeshwa Coco
beach kati ya Manchester United na Aston Villa itakayochezwa jumapili.
Rashid
Jacob Kagomola na Dickson Lyatuu ni washindi wa kwanza wawili wa promosheni ya
Mimi ni Bingwa waliojishindia tiketi za kwenda Old Trafford, ambapo zawadi
zaidi ya shilingi milioni 40 tayari imetolewa kwa ajili ya washindi wa kila
siku na kila wiki.
Mmbando
alisema kuwa bado kuna zawadi nyingi zaidi kushindaniwa katika promosheni, na
kuongeza kuwa ili mteja kushiriki anatakiwa kutuma ujumbe mfupi (SMS) wa neno
"BINGWA" kwenda namba 15656.
Aidha,
alisema Airtel imeweka vituo mbali mbali ambavyo washabiki wa Man U wataweza
kuangalia mechi za Manchester United moja kwa moja (live) kupitia luninga
kubwa, na kutaja vituo hivyo kuwa ni Mbeya - Shaba Pub, Mwanza - Shooters Pub,
Dodoma - Four ways, Dar es Salaam - Coco Beach, Morogoro - Nyumbani Lounge na
Arusha - Empire Sports bar.
Mwaka
2011 kampuni ya mawasiliano ya Airtel Tanzania ilizindua mpango wa kuvumbua
vipaji katika soka kwa ushirikiano na klabu ya Manchester United, uliolenga
kuvumbua vipaji na kuviendeleza katika mpira wa miguu Tanzania.
Cole
amekuwa na dhamira ya kuonyesha uzoefu wake kwa wachezaji nyota wanaochipukia
ikiwa ni kama njia ya kuunga mkono maendeleo ya mchezo wa mpira wa miguu
duniani.
0 comments:
Chapisha Maoni