COASTAL UNION ULIVYOIGAGADUA YANGA NA KUTWAA UBINGWA WA UHAI CUPRAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Jamal Malinzi amesema watakaa na wadhamini wa mashindano ya Uhai ili yachezwe kwa mfumo wa ligi, sambamba na ligi Kuu ya Tanzania Bara
Malinzi aliyasema hayo juzi wakati akifunga fainali za mashindano ya kombe la Uhai zilizofanyika katika Uwanja wa Chamazi ulionje ya jijini la Dar es Salaam.

“Tunawapongeza Uhai kwa kufadhili mashindano haya ambayo yanalengo la kuibua vipaji ila shirikisho litakwenda kuzungumza nao ili mashindano haya yachezwe kwa mfumo wa ligi sambamba na ligi kuu ya Tanzania ili kutoa wigo mpana kwa vijana kuonyesha uwezo wao”, alisema Malinzi.

Pia alisema mfumo wa sasa wa makundi unazikosesha fursa timu zingine kuendelea mbele kwani inawezekana kabisa kama mchezo wa kwanza timu inafungwa mchezo wa pili inafanya vizuri.

Katika fainali hizo timu ya Coastal Union ilitwaa ubingwa kwa kuifunga Yanga mabao 2-0 na kuzawadiwa kikombe na fedha taslimu 2, 500, 0000 huku Yanga wakiambulia 1,500,000.
Pia Azam Fc ilichukua nafasi tatu na kuzawadiwa 1,000,000 baada ya kuifunga Mtibwa Sugar penati 4 kwa 3 baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 katika muda wa dakika 120.


Kocha wa Mtibwa Sugar, Zuberi Katwila alipata zawadi ya kocha bora huku Ally Kabunda wa Ashanti United akipata zawadi ya mfungaji bora baada ya kufunga mabao 9 na Ruvu Shooting ikipewa zawadi ya timu bora.
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List