DVD MPYA YA BONDIA FRANSIC MIYEYUSHO IKIWA IMESHEHENI MAPAMBANO
MBALIMBALI YA NGUMIMWAKA huu unaonekana kuanza vizuri kutokana na
wanamichezo na wasanii mbalimbali kuonesha nia
mbalimbali.
Yawezekana ni mapema kusema hivyo, lakini dalili za
mvua ni mawingu na ishara za moshi mweupe
zimeanza kuonekana miongoni mwa wanamichezo wetu.
Hivi karibuni bondia, Francis Miyeyusho
amefanya kitu cha hatari kwani kama si
kujiamini huwezi kufanya kitu kama hicho.
Wakati kwa mara ya kwanza inatangazwa Miyeyusho
anapigana na David Charanga kutoka Kenya katika
pambano la kimataifa lisilo la ubingwa, sikushangaa ila
nilipigwa na butwaa kusikia pambano hilo kaliandaa
mwenyewe.
Unaweza kuona bondia Miyeyusho ni mtu wa aina gani
mpaka kupata ujasiri wa aina hiyo kwa kukubali
kuingia gharama bila kujali kama atapigwa au
vinginevyo.
Lakini Mungu si Athumani, Miyeyusho
aliibuka na ushindi kwa kumtwanga Joshua Amakulu
kwa KO raundi ya pili katika pambano lililofanyika kwenye Ukumbi
wa New Msasani Beach, Dar es Salaam.
Miyeyusho ililazimika kupigana na huyo badala ya
mpinzani wake wa awali, Charanga kufiwa na mama
yake mzazi na kuomba kuondolewa katika pambano
hilo.
Katika pambano hilo Miyeyusho alimpiga Amakulu kwa
KO raundi ya pili na mara baada ya pambano,
kulilipuka kwa shangwe na nderemo huku kila mtu
akimpongeza kwa kazi nzuri ya kumpiga mpinzani
kabla ya kumaliza raundi zote 10.
Akizungumza baada ya mpambano huo, Miyeyusho
anasema kuwa anamshukuru Mungu kwa kufanikiwa
kushinda pambano hilo pia kwa sapoti kubwa aliyopata
kutoka kwa viongozi na mashabiki wa ngumi.
"Niliamua kufanya kitu kama hiki ili kujiongezea kipato
na mafanikio katika kazi yangu, si rahisi kujitoa kama
hivi kwa kuandaa kitu ambacho hujui itakuwaje
mwisho wa siku," anasema Miyeyusho.
Anasema alifikiria kwa umakini nini afanye katika
kumaliza mwaka na kuukaribisha mwaka mpya ndipo
alipopata wazo la kuandaa pambano kama hilo ambalo
limempa sifa.
Miyeyusho anashikilia mkanda wa UBO na kwamba
kwa ushindi huo anaimani atakuwa katika nafasi nzuri
ya kutafutiwa pambano la kuwania ubingwa wa Dunia.
Bondia huyo ambaye anarekodi ya kucheza
mapambano 49 huku akishinda 27 kwa ‘KO’, kupoteza
saba na mengine 15 akishinda kwa pointi, amesema
siri kubwa ya kupata mafanikio ni kujituma mazoezini.
Miyeyusho anasema soko la ngumi kwasasa limepanda
na endapo kama bondia anakuwa na malengo mazuri
katika maisha yake, lazima atafanikiwa na kupiga
hatua.
Anasema ngumi za siku hizi zimepanda bei
ukilinganisha na zamani bondia alikuwa anapanda
ulingoni kutangaza jina lake lakini kwasasa bila fedha
hakuna bondia ambaye atakubali kupanda ulingoni
kuzichapa bure.
Anasema yeye binafsi anapopata pambano hapa
nchini, anataka alipwe fedha zisizopungua sh. milioni
10 kutokana na ugumu wa mchezo huo.
“Unaweza kufa kutokana na mchezo huu, ni wa hatari
hivyo bila ya sh. milioni 10 sipandi ulingoni.Kwa sasa
nimeshakuwa bondia mzoefu," anasema Miyeyusho.
Bondia huyo ambaye pia ni bingwa wa WBF, IBU Afrika
anasema kiwango chake kinamridhisha lakini
anapenda kufikia kama cha, mabondia wa tanzania
walitwaa ubingwa dunia, Francis Cheka na Mmbwana
Matumla kutokana viwango vyao kuwa juu hapa
nchini.
Miyeyusho anasema kati ya nchi ambazo amepita
kufanya kazi na kugawa kichapo kwa mabondia wa
nchi hizo ni pamoja na Zambia, Kenya, Malawi,
Uganda, Marekani na nyinginezo.
Nini kilimfanya awe bondia
Kufanya vizuri kwa kaka yake, Ramadhani Miyeyusho
ndio sababu kubwa iliyomfanya aingie katika mchezo
huo na pia alikuwa akiupenda tangu akiwa mtoto.
“Nilivyomaliza masomo yangu nikaona nifanye kile
ninachokipenda hivyo nikaamua kuingia rasmi kwenye
ngumi, ili niweze kutimiza ndoto zangu za kuwa
bondia mkubwa Tanzania na nchi za jirani,” anasema.
Pamoja na hayo, anaishauri serikali iangalia na upande
wa pili siyo kila siku inaangalia mchezo wa soka peke
yake ambao hauna mchango wa kutosha kama ilivyo
michezo mingine hasa ngumi.
Anasema anaimani kama wataandaliwa vizuri ka
ma
Anasema anaimani kama wataandaliwa vizuri ka
wanavyofanyiwa wachezaji wa timu ya Taifa (Taifa
Stars), watapeperusha vizuri bendera ya taifa katika
mashindano mbalimbali.
Miyeyusho kwasasa yupo katika maandalizi ya kupambana na bondia Mmarekani katika pambano la kuwania ubingwa wa Dunia wa WBF.
“Bado
sijajua ni bondia gani ambaye nitapigana naye ila nimeambiwa nijiandae
kwa pambano hili nafikiri litafanyika mwezi wa pili naomba sapoti tu kwa
wadau na wapenzi wa ngumi ili niweze kukamilisha ndoto zangu,”anasema
0 comments:
Chapisha Maoni