Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Twalib 'Teacher'
(kushoto)
MTANDAO wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) umeandaa
kongamano la umoja na mshikamano linalofanyika Januari 17 (Ijumaa)
kwenye viwanja vya hoteli ya Lamada ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Rais Jakaya Kikwete.
Mwenyekiti wa SHIWATA,Caasim Taalib alisema madhumuni ya
kongamano hilo ni kuhamasisha umoja kati ya wasanii ili kujenga uwezo na
nguvu ya kumaliza matatizo yao ya kiuchumi.Katika kongamano hilo Shiwata itazingua mpango maalum ambao utawezesha wasanii kupata misaada ya fedha za kutengeneza filamu,kurekodi muziki,kuwezesha timu na vikundi mbalimbali kununua vifaa vya ichezona kuwapatia nauli ya usafiri ndani na nje ya nchi kwa shughuli za michezo na sanaa.
Katika Mpango huo Shiwata pia itatoa fedha kwa mrithi wa msaniii kamaatakufa, akiugua au kulazwa kwa siku tatu katika hospitali zinazotambuliwa na Serikali.
Alisema Shiwata pia itatoia misada kwa wasanii wanaotaka kuoa au kuolewa ambako kila mwanachama atachangia sh. 1,000 kwa ajili ya kugharamikia mazishi ya msanii kununua sanduku n usafiri.
Sjiwata
ina ekari 300 za makazi katika kijiji cha Mwanzega Mkuranga ambapo hivi
sasa kuna nyumba 40 zilizojengwa kwa nguvu ya wasanii wenyewe na ekari
500 za kilimo.
0 comments:
Chapisha Maoni