Ndugu Matei Joseph Misegege Muhumiwa aliyengeneza Hati feki ya Kusafiria iliyokamatwa jana akiwa ameshikiliwa katika ofisi za uhamiaji Wilaya ya Temeke.
Kijana Halfani Rashidi ambaye aliyetengenezewa Hati Feki ya kusafiria na Matei Joseph Misegege akiwa ameshikiliwa na Maofisa wa Uhamiaji Wilaya ya Temeke jana hasubui akitoa maelezo juu ya kukamatwa kwake
Afsa Uhamiaji Wilaya ya Temeke Ndugu DCI Jaffary S. Kisesa akifafanua kwa umakini Hati ya kusafiria ilio feki kwa Wahandishi wa habari iliyokamatwa jana hasubi.
Mtengenezaji wa Hati feki ya Kusafiria Ndugu Matei Joseph Misegege Mkazi wa magomeni amekamatwa leo Majira ya saa 5 Hasubui na anashikiliwa katika ofisi ya Uhamiaji Wilaya ya temeke.Akiongea na wahandishi wa Habari,Afsa Uhamiaji Wilaya hii ya Temeke Nd.DCI.Jafarry S.Kisesa alisema kuwa mtuhumiwa alikamatwa leo majira ya hasubui na alimtapeli kwa kumtengenezea kijana Halfani Rashidi mkazi wa huko magomeni. Alipohojiwa Mtuhumiwa alikiri kuhusika na tukio ilo na kumuomba Afsa uhamiaji Nd.DCI Jafarry S.Kisesa msamaha na kumuomba hawezi kurudia tena kwani ni Shetani alimpitia.Alisema ya kuwa,Ndugu Halfani Rashidi alimkabizi Sh.taslimu Alfu Sitini (60000\=) zikiwa ni garama za utengenezaji wa hati hiyo wakati Garama harisi ya Kiserikali ya kutengeneza Hati ya Kusafiria ni Shilingi Alfu Kumi (10000\=). Akiongea na wahandishi wa habari Kijana ambaye anahusika na kufanyiwa kitendo hicho alisema ya kuwa,Nd.Matei joseph Misegege ni Mwanamuziki na alimwambia ya kuwa yeye ni mtahalamu wa kutengeneza hati hizo na kila siku huwa anawatengenezea watu mbalimbali ndipo alimpatia fedha hizo na kumpatia Hati feki hiyo ndipo yeye akaamua kufika katika eneo la Ofisi za uhamiaji Temeke kwa nia ya kupiga muhuri wa uhamiaji ndipo dada mmoja aliibaini kuwa ni feki.Baada ya kuibaini kuwa ni feki kijana Halfani aliwekwa chini ya ulinzi ndipo maafisa wa uhamiaji walimuhamuru kijana huyu akawaonyeshe alikoipata hati hiii. Walipofika kule magomeni ndipo Ndugu Matei Joseph Misegege aliwekwa chini ya ulinzi na kufikishwa katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo Wilayani Temeke.Mtuhumiwa na kijana wanashikiliwa na Ofisi hii na watapelekwa katika Ofisi kuu ya Mkoa wa Dar-Es-Salaam kwa kufikishwa Mahakamani. Akitoa wito Afsa Uhamiaji wa Wilaya ya Temeke Ndugu DCI Jaffary S.Kisesa,aliwataka wananchi kuwa makini na watu mataperi na kuwaomba kuwa ni vema kama wanahitaji huduma ya kupata hati halisi ya kusafiria waweze kufika katika Ofisi za Uhamiaji zilizopo karibu wilaya zote za Dar-Es-Salaam.
0 comments:
Chapisha Maoni