MWENYEKITI CHADEMA AITABIRIA CCM USHINDI WA KISHINDO KALENGA*Asema ni kwa wananchi kupania kuimininia kura
*Kwa sababu ikiahidi inatenda
*Lakini Chadema porojo tu
NA BASHIR NKOROMO, KALENGA

MWENYEKITI wa Kitongoji cha Lupembelwasenga, Jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, kwa tiketi ya Chadema, Ezekiel Kibiki, ameitabiria CCM kuimiminiwa kura za kishindo na wananchi wa kitongoji hicho katika uchaguzi mdogo wa
ubunge utakaofanyika jimboni humo Machi 16, mwaka huu.

Amesema, uhakika huo anao kutokana na yeye na wananchi wengi wa kitongoji hicho kubaini kwamba CCM ikiahidi jambo inatekeleza na ndiyo yenye ilani inayotekelezwa kwa sasa tangu ilipopewa ridhaa na wananchi ya kuongoza nchi katika uchaguzi mkuu uliopita, tofauti na Chadema ambao alidai ahadi zao ni za uongo na hawana kazi ya kufanya katika shughuli za maendeleo.

Mwenyekiti huyo wa kitongoji kwa tiketi ya Chadema, alisema, hayo leo, Machi 4, 2014, kabla ya kutangaza kuihama Chadema na kujiunga na CCM, katika mkutano wa hadhara wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye kitongoji hicho, kumnadi mgombea wa CCM, Godfrey Mgimwa.

"Hivi sasa natangaza kuhama Chadema, na nina kuhakikishieni kwamba wapo watu wengi nyuma yangu ambao tumeachana na chama hicho na sote kwa jumla tumeahidi wananchi wa kitongoji chetu kuifanya CCM iibuke na ushindi wa kishindo kwa kuimwagia kura zetu nyingi katika uchaguzi huu, anayefikiri natania asubiri ataona baada ya uchaguzi", alisema Kibiki.

Kibiki alisema, yeye na wenzake wameamua kuachana na Chadema baada ya kubaini kwamba, maneno ambayo yamekuwa yakitolewa na viongozi wa chama hicho ni ulaghai mtupu ambao ukifuatwa unawapotezea muda wananchi katika kujiletea maendeleo.

Alisema, baada ya kutafakari kila mmoja kwa wakati wake, wamebaini kwamba, CCM ndicho chama chenye uhakika wa kusimamia maendeleo yao, kwa sababu kiliwaahidi kujengwa barabara nzuri na sasa ipo, mbali na mambo mengine ambayo yametekelezwa kupitia aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo la Kalenga na Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa ambaye alifariki dunia Januari Mosi, mwaka huu.

Baada ya kutangaza kuachana na Chadema na kujiunga na CCM, Kibiki alikabidhi kadi yake, kwa Mwenyekiti wa CCM Iringa Vijijini Delfina Mtavilalo, hatua iliyofuatiwa na wanachama wengine tisa wa Chadema kutoka kitongoji hicho nao kukabidhi kadi zao kwa Mwenyekiti huyo.

Akizungumza na wananchi kwenye mkutano huo, Mgombea wa CCM katika uchaguzi huo wa Kalenga, Godfrey Mgimwa alisema, anatambua changamoto zinazowakabili wananchi wa jimbo hilo, ndiyo sababu amejitolea kuipeperusha bendera ya CCM ili akipata fursa ya kuchaguliwa asimamie kuzitatua.

Mgimwa alisema, miongoni mwa changamoto ni uendelezaji wa ujenzi wa zahanati na shule katika Kitongoji hicho, ambao ulikuwa umeanzishwa na Mbunge wa zamani Dk. Mgimwa.

Alisema, ana uhakika kwa kupata ushirikiano wa wananchi na mwongozo wa ilani ya CCM ya mwaka 2010, ana uhakika changamoto hizo na nyingine zilizopo atapambana nazo hadi kuhakikisha zinapungua au kwisha kabisa.
 Katibu wa CCM mkoa wa Mtwara, Shaibu Akwilombe akimnadi Godfrey Mgimwa, katika mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Kalenga, Iringa Vijijini, uliofanyika katika kijiji cha Kikombwe leo...PICHA ZAIDI>BOFYA HAPA
Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List