Diwani wa kata ya kibiti wilayani rufiji mkoani pwani Mh.Amidu Ungando amemlalamikia mkuu wa mkoa Mh.Mwantumu Mahiza kwa kuhamisha gari la wagonjwa kutoka kituo cha afya kibiti na kulipeleka kwenye zaanati ya nyamisati
Diwani huyo alidai kwamba gari hilo lilitolewa kama msada na taasisi ya afya..ya Ifakara (IHI) mnamo Mei 2 kwa lengo la kuwaudumua watu wengi ktoka kata mbali mbali za wilaya ya Rufiji..
.
"hili gari la wagonjwa lili tolewa kwa ajili ya kituo cha afya cha kibiti,inakuaje mkuu wa mkoa analipeleka kata nyingine tena kwenye zahanati? ninavyo vielelezo vya makabidhiano kutoka IHI ," ali lalamika Diwani Ungando mbele ya wananchi wake..
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa pwani Mh.Mwantumu Mahiza amesema uwamuzi wa kuamisha gari hilo,ulitokana na ukweli kwamba kituo hicho afya cha Kibiti tayari kina gari lingine hivyo serikali ilionelea ni vyema na Zahanati ya Nyamisati nayo ikapatagari la wagonjwa..
"kata ya Nyamisati wanapata shida kubwa ya usafiri wa kuwafikisha wagonjwa kwenye zahanati na vituo mbalimbali vya afya,"alisema mkuu huyo wa mkoa.
Mwananchii wa kata ya Kibiti akilalamika kwa kata
yao kunyang'anywa gari la wagonjwa
Wananchi wa kata ya Kibiti wakimsikiliza diwani wao
(hayupo pichani)
Mkuu wa Mko wa pwani Mh.Mwantum Mahiza
RAIS DKT.SAMIA SULUHU HASSAN ATOA POLE AJALI YA KARIAKOO
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan
akitoa salamu za pole kwa waathirika wa ajali ya kudondokewa na gorofa
Kariakoo Jij...
Wiki 1 iliyopita
Blogger Comment