Serikali ya Mali imepuuza mzozo
unaotokota kati yake na shirika la fedha duniani IMF kuhusu hatua ya
kumnunulia Rais wa nchi hiyo ndege kuu kuu kwa kima cha dola milioni
arubaini, hata baada ya kuahidi kulipatia swala la umasikini kipaombele.
Maafisa wa Mali watahojiwa hii leo katika mkutano wa wafadhili hao wa kimataifa.Mwakilishi wa IMF nchini Mali, Anton Op de Beke, aliambia BBC kuwa hawajaelezwa kikamilifu kwa nini serikali ilifanya hivyo.
Lakini waziri wa mawasiliano wa nchi hiyo ,Mamadou Camara, alisema kuwa walikuwa wameieleza serikali kuhusu mpango wa kununua ndege hiyo na kuwa nchi hiyo ina uhusiano mzuri tu na shirika la IMF.
Wahisani wa kimataifa, ambao wako nchini Mali, wanatarajiwa kuhoji ununuzi huo pamoja na kandarasi ya ulinzi iliyotolewa na nchi hiyo na ambayo itaigharimu serikali dola milioni miambili.
Mwaka mmoja uliopita , wahisani waliahidi kuipa Mali dola bilioni nne kuisaidia serikali kukarabati nchi baada ya vita.
Blogger Comment