Mamia ya watalii kutoka
Uingereza waliokuwa kisiwani Mombasa Kenya wamelazimishwa kurejea makwao
baada ya serikali ya nchi hiyo kutoa tahadhari ya tishio la
mashambulizi ya kigaidi nchini Kenya.
Kampuni zinazopanga safari za watalii kutoka
Uingereza Thomson na First Choice zilifutilia mbali safari zote
zilizokuwa zimepangwa kuwaleta watalii Mjini Mombasa hadi mwezi Oktoba
zikihofia usalama wao.Tahadhari hiyo kutoka kwa serikali ya Uingereza imesema kuwa wanamgambo wa kiislamu kutoka nchi jirani ya Somalia al-Shabab huenda wakafanya mashambulizi nchini Kenya.
Ilani hiyo iliwaonya raiya wote wa Uingereza ambao wako nchini Kenya kwa shughuli ambazo si za dharura waondoke takriban kilomita 60 kutoka kwenye mpaka kati ya kenya na Somalia.
Kampuni ya utalii ya Thomson imewarejesha nyumbani kundi la kwanza la watalii huku waliosalia wakiratibiwa kuondoshwa ijumaa.
Watalii walishauriwa wasizuru kisiwa cha Mombasa huku wakishauriwa kuwa Diani beach na Uwanja wa ndege wa Moi Mombasa ni salama kwao.
Al Shabab
Al-Shabab imeimarisha mashambulizi katika eneo hilo katika siku za hivi punde kundi hilo likisisitiza kuwa linalipiza kisasi vitendo vya majeshi ya Kenya nchini Somalia .
Blogger Comment