Serikali ya Tunisia imefutilia mbali mkutano wa dharura wa mataifa ya kazkazini mwa Afrika ili kuzungumza kuhusu mzozo wa kisiasa nchini Libya.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Tunisia Mokhtar Chao-uachi amesema kuwa wameshindwa kupata mtu atakayeiwakilisha serikali ya Libya kufuatia makabiliano ya mamlaka katika serikali hiyo
Mataifa matano ya muungano wa mataifa ya kiarabu yalitarajiwa kukutana hii leo katika mkutano mkubwa ambao ungehusisha Libya ,Umoja wa Mataifa ,Marekani na muungano wa Ulaya.
Blogger Comment