CCM yajipanga kukomboa majimbo yote ya Dar

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Dar es Salaam kimesema kimejipanga kuhakikisha kinarudisha majimbo yote ya uchaguzi katika mkoa wa Dar es Salaam katika uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwakani.

Aidha, chama hicho kimesema kitahakikisha kinachukua nafasi nyingi katika uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwaka huu kabla ya uchaguzi mkuu ujao.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki na Katibu Mwenezi wa Chama hicho mkoa wa Dar es Salaam, Juma Simba, alipokuwa akizindua matawi ya mashina mapya Kata ya Upanga Magharibi.

Simba alizindua mashina mapya matatu katika kata hiyo ambayo ni Gadafi, Upanga Magharibi na Tambaza Jumbe ambako walipata wanachama wapya 300 na kuwagawia kadi.

Simba aliwataka wanachama wa chama hicho kutafuta mitaji ya wanachama na kata ya Upanga itaendelea kuwa ngome kuu ya Chama hicho.

Majimbo mawili yanayoshikiliwa na upinzani katika mkoa wa dare s salaam ni Ubungo ambalo mbunge wake ni John Mnyika (Chadema) na Kawe ambalo linaongozwa na Halima Mdee (Chadema).

Hata hivyo, Simba hakueleza mbinu zitakazotumika kuyakomboa majimbo hayo.

Abdulahaman Kinana
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List