MFANYAKAZI WA NYUMBANI MDOGO ANYANYASIKA.



mtoto Ketina Anodi akiwa na mjumbe wa nyumba kumi Bi.Verdiana Saimoni,aliyeweza kumsaidia mtoto huyo ili apate haki zake.
akinunuliwa ndala(kandambili) na Polisi wa kituo kidogo cha Sigara.

Mama anayeishi naye mtoto anayefahamika kwa jina Betrice Satibulanga

mtoto akionyesha mkono wake uliovimba kwa ajili ya kupigwa,pia alisema alikuwa anapigwa hadi kuvimba kwenye makalio.

kituo kidogo cha polisi alipofikishwa ili kupata msaada na baadae walipelekwa kituo cha polisi changombe

Mhusika anayehusika na kumtesa mtoto alijificha ili sura isionekane anayejulikana kwa jina la Maxi Katikilo
 Polisi wa kituo cha changombe Engelbert Kiondo,SACP-Senior,Assistant commissioner of police-RPc TEMEKE,Amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.Ametoa onyo kwa jamii kuacha vitendo vya ukatili kwa watoto na atakeyebainika sheria itachukua mkondo wake.

Pamoja na Serikali kupiga vita ajila kwa wa watoto na unyanyasaji wa binadamu,bado watu wamekuwa wakiwatendea vitendo vya kinyama wafanyakazi wa ndani wenye umri mdogo.Haya yametokea maeneo ya Lumo Yombo vituka mtaa wa Sigara.mtoto huyo alifahamika kwa jina la KETINA ANODI mwenye umri wa miaka 14,kabila la Mkaguru.Akiongea na mwandishi wa blog hii amesema Bosi wake alituma nauli bila kumjua yeye wala wazazi wake kwa kumtumia mfanyakazi mwengine anayeitwa Evaline Cristopher baada ya kufika DAR ES SALAAM TAREHE 7-04-2014.Msichana huyo anadai toka afike hajawahi kulipwa mshaara wala kununuliwa viatu hivyo alikuwa anatembea bila viatu pia ameeleza kuwa Bosi wake alikuwa akimpiga mara kwa mara na hata chakula alikuwa akipata mlo mmoja kwa siku.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List