Waasi 100 wauawa Kordofan,Sudan

Jeshi nchini Sudan linasema kuwa limewaua zaidi ya waasi 100 katika jimbo la Kordofan Kusini.

Msemaji wa jeshi Sawarmi Khaled Saad anasema kuwa mauaji hayo yalifanyika wakati wa mapigano yaliyodumu muda wa saa tatu ya kuzima shambulizi eneo la El Atmor.

Waasi kutoka kwa kundi la (Sudanes Peoples Liberation Movement North) walithibitisha shambulizi hilo na kusema kuwa ni wapiganaji watatu tu waliouawa.

Kundi hilo limekuwa likiipiga vita serikali ya Khartoum eneo hilo kwa kipindi cha miaka 20 sasa

Umoja wa Mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni moja wameathiriwa na vita nchini humo.

Vita hivyo vimezuka wakati Rais Salva Kiir na hasimu wake Riek Machar wa Sudan Kusini wakitarajiwa kukutana leo kwa mazunguzmo ya amani , ukiwa mkutano wa kwanza katika kipindi cha mwezi mmoja na wa pili tangu vita kuzuka nchini Sudan Kusini.

Mazungumzo ya kwanza kujaribu kuleta amani kati ya pande zinazohasimiana yamecheleweshwa kwa zaidi ya mara maoja.

Wajumbe kutoka pande zote wamekuwa wakikutana katika hoteli za kifahari nchini Ethiopia tangu mwezi Januari ingawa hakuna hatua zozote zimefikiwa za suluhu ya kudumu huku pande zote daima zikijadili kuhusu swala tete la ajenda.

Mkataba wa kusitisha vita uliotiwa saini na Kiir na Machar tarehe 9 mwezi Mei,umekuwa ukikiukwa na kuvunjwa na pande zinazozozana kwenye mgogoro huo ambao tayari umesababisha vifo vya maelfu na kuwalazimisha wengine milioni moja nukta tatu kutoroka makwao.

Waziri wa mambo ya nje wa Ethiopia Tedros Adhanom amesema kuwa pande zote husika kwenye mgogoro huo zimetenda uhalifu wa kivita.

Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List