SERIKALI YASHAURIWA KUTUNGA SERA YA KUDHIBITI POMBE


.



DSC_0279
Banda la Mtandao wa mashirika yapatayo 30 ya kupambana na matumizi ya kupita kiasi ya pombe nchini (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana duniani.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).

Na Mwandishi Wetu
SERIKALI imeshauriwa kutunga sera madhubuti ya udhibiti wa pombe katika jamii ili pamoja na mambo mengine kuhakikisha vijana wanalindwa dhidi ya bidhaa hiyo kwenye soko.
Akizungumza na Moblog Tanzania jijini Dar es Salaam katika viwanja vya chuo kikuu wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya vijana, Msemaji wa Mtandao wa kupambana matumizi ya pombe kupita kiasi (Tanzania Network Against Alcohol Abuse) Bw, Mathias Kimiro amesema kwamba kuna umuhimu wa serikali kutunga sera mpya ya pombe ili kuzuia madhara kwa vijana na taifa kwa ujumla.

“Kwa kawaida matumizi ya pombe kupita kiasi ina madhara makubwa katika afya ya mtumiaji lakini vile vile ina madhara kwenye familia kupitia kaya moja moja na kusababisha mateso kwa familia hasa watoto,” amesema Bw Kimiro

Amesema kwamba umuhimu wa kuwa na sera madhubuti ya kudhibiti pombe katika jamii ni kuangalia upya ni kwa kiwango ngani matangazo ya pombe yanavyohamasisha unywaji kupita kiasi kwenye jamii. Bw Kimiro aliongeza kwamba mashirika yasiyo ya kiserikali yataendelea kuwakumbusha mamlaka zinazohusika umuhimu wa kuwa na sera ya kudhibiti pombe katika jamii pamoja na kuangalia madhara ya matangazo kwa wasomaji wa mabango.
DSC_0300
Mkurugenzi Mtendaji wa Makangarale Youth Theatre, ambao ni taasisi chini ya Tanzania Network Against Alcohol Abuse (TAAnet), Bw. Ismael Mnikite akifafanua jambo kwa Mgeni Rasmi kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Vijana na Michezo, Bibi Venerose Mtenga wakati wa maadhimisho hayo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List