DAWASA NA MGOGORO WA KUTUMIA KINYUME MSAADA WA KIASI KIKUBWA CHA FEDHA KUTOKA BENKI YA DUNIA

Wakati benki ya Dunia ikitoa shilingi Bilioni kumi kwa ajili ya fidia kwa wakazi wa maeneo ya Bwila juu,Bwila chini na Mkoani Morogoro ili kupitisha mradi wa bwawa la maji wa kidunda,Wananchi hao wamelalamikia malipo hayo duni,yanayokadiriwa kufikia Milioni 280 tu.

Bwawa linalotarajiwa kujengwa litakuwa na ujazo wa mita Milioni 190,na litasaidia upatikanaji wa maji kwenye mikoa ya Dar es salaam,Pwani na Morogoro.

Wananchi wakieleza kwa masikito ya kile walichodai kuwa ni uonevu na malipo Duni ya fedha za fidia za kupitisha mradi wa bwawa hilo,ambapo wakazi 2068 wanatakiwa kuhamia makazi mapya yaliyopo eneo la Bwilla.

Jumla ya viwanja 1000vimekwishapimwa,na wakazi hawa wanaotakiwa kuhama,wanalipwa hundi za fidia za kati ya shilingi elfu nne hadi milioni tano,Hatua inayowafanya wakazi hao kuhoji uhalali wa malipo hayo duni.

Baadhi ya viongozi waliohudhuria mkutano wa walalamikaji hao nao wakatakiwa kutolea ufafanuzi malalamiko hayo,lakini wakasema hawakuwa na maelezo ya ndani zaidi kuhusu malipo,Bali ni DAWASA ambao ndio wasimamizi wakuu wa mradi huo.

Mwandishi wa Blog akiwa ndani ya ofisi ya DAWASA,zilizoko Mwananyamala jijini Dar es salaam,na kukutana na msemaji msaidizi aliyejitambulisha kwa jina moja tu la Meki,ambaye alijibu kwa Lugha ambayo si nzuri kwa Waandishi.

Mmoja wa wananchi waliathiriwa na malipo duni ya DAWASA

Mmoja wa wananchi waliathiriwa na malipo duni ya DAWASA akionyesha Hundi aliyolipwa.

Baadhi ya maeneo yanayotakiwa kupisha ujenzi wa Bwawa la maji wa kidunda

Wananchi wakisikiliza kwa makini

Wananchi wakisikiliza kwa makini

Mkuu wa wilaya ya MOROGORO Mh:Saidi Amanzi

Mh;INNOCENT KALOGERIES mbunge wa MOROGORO kusini

Msemaji msaidizi wa DAWASA ambaye hakuweza kutoa majibu yanayofaa kwa kujibu kwa kauli chafu  baada ya kuhojiwa maswali.alifanikiwa kujulikana kwa jina la MEKI

AFISA HABARI WA DAWASA BI;NELY MSUYA ambaye hakuweza kuongea chochote juu ya malipo ya fidia kwa wananchi.

Nembo ya DAWASA

Mh;JUMA MANYILE(mwenyekiti kijiji cha kiburumo)

Baadhi ya hundi zilizotolewa kwa wananchi hao.

Baadhi ya hundi zilizotolewa kwa wananchi hao.
Mmoja wa wananchi waliathiriwa na malipo duni ya DAWASA akitoa malalamiko yake kwenye mkutano.

Baadhi ya hundi zilizotolewa kwa wananchi hao.


 Baadhi ya hundi zilizotolewa kwa wananchi hao.

Wananchi wakisikiliza kwa makini

Share on Google Plus

About GLORIA MATOLA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
Chapisha Maoni

Watch the Video Here

Loading...
Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

Google+ Followers

TANGAZO

My Blog List