Mjumbe wa halmashauri kuu Taifa amewataka wanaharakati
kuonyesha uelewa wao katika kuongelea
Bunge maalumu vizuri na sio kushikiliwa na vyama vya siasa kulazimisha Rais
asimamishe Bunge la katiba linaloendelea kwa manufaa ya watu wachache.Pia
ameomba Amani katika kipindi hiki cha mpito na kufanya ipatikane katiba itakayo
kidhi matakwa ya Watanzania.
Amesema CCM inazingatia sana uadilifu na kupenda kuwa karibu
na wananchi hivyo ushirikishwaji ni kipaumbele ndani ya Chama cha mapinduzi.
Katika kujazia hayo amesema CCM ina utaratibu mzuri wa
kuchagua viongozi hivyo amewataka Watanzania wachague viongozi wazuri ili waweze kutumikia Taifa.Na kutoa
ushauri kwa vijana kutopenda kukimbilia mjini na kutambua fursa zilizopo
mikoani na kujiingizia kipato.
KALIST .J. LYIMO,Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa.
0 comments:
Chapisha Maoni