Wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi imesema itaendelea
kutekeleza hatua mbalimbli za kukabiliana na changamoto za ufungufu wa vifaa
vya ukaguzi wa mashule,ili kuboresha zoezi hilo linalolenga kuweka viwango sawa
vya kitaaluma na mazingira na kila shule kufikiwa kwa wakati.
Zoezi la ukaguzi wa shule za msingi na Sekondari,limekuwa likikabiliwa na
changamoto mbalimbali,kubwa ikiwa ni upufungufu wa watendaji na vifaa
ikilinganishwa na idadi ya shule zilizopo hapa nchini.
Miongoni mwa hatua ambazo tayari wizara hiyo imechukua ni
kuwashirikisha wadau wa sekta ya elimu kitaifa na kimataifa ili kuziba pengo la
upungufu wa vifaa na watendaji,hivyo kulifanya hilo kuwa gumu kwa kushindwa
kuzifikia shule zote,suala ambalo ni kunyume na malego.
Aidha,Wizara hiyo imewataka wadau kuendelea kuunga mkono
juhudi za Serikali za kukabiliana na Changamoto za kielimu,hususani kwenye
uchangiaji,wakati ambapo wizara hiyo inatekeleza mpango wa maendeleo makubwa
sasa,BRN,ili uwe na mafanikio.
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya miaka kumi ya shule ya
msingi ya Heritage ya jijini Dar es salaam ambapo nae,mkuu na makamu mkuu wa
shule hiyo nao wakazungumzia umuhimu wa wanajamii kushiriki katika kuendeleza
sekta ya elimu.Baadhi ya wanafunzi nao walionyesha uwezo wao wa kujua baadhi ya masuala yanayoendelea sasa hapa nchini.Pamoja na miaka kumi,shule hiyo iliadhimisha mahafali ya saba ya darasa la saba,ambapo wahitimu 62 walifikia tamati ya elimu ya msingi.
Wanafunzi wa shule ya AWALI na MSINGI HERITAGE wakishuhudia mahafali ya wanafunzi wa Darasa la Saba.
Wahitimu wa Darasa la Saba wa Shule ya msingi HERIATAGE wakipita mbele ya Hadhara.
Baadhi ya wanafunzi wakionyesha maonyesho mbalimbali siku ya Mahafali ya Darasa la Saba.
Baadhi ya wanafunzi wakionyesha maonyesho mbalimbali siku ya Mahafali ya Darasa la Saba.
Sara Mlaki,Kaimu Mkurugenzi wa shule za Msingi
Elia kabazo,Mkuu wa Shule ya AWALI na MSINGI HERITAGE
Jefta Chambo,Makamu Mkuu wa shule
Moses Mkindi,Mhitimu wa Darasa la Saba.
Christabella George,Mhitimu wa Darasa la Saba.
Baadhi ya wanafunzi wakionyesha maonyesho mbalimbali siku ya Mahafali ya Darasa la Saba.
Mariaam Majura,Mhitimu wa Darasa la Saba.
0 comments:
Chapisha Maoni