Maafisa nchini Kenya wameifunga Madrassa





Maafisa nchini Kenya wameifunga Madrassa au shule ya mafunzo ya dini nchini humo kwa madai kuwa inafunza masomo ya itikadi kali.
Madrassa hiyo iliyo mjini Machakos, Mashariki mwa Nairobi, imechukuliwa hatua hiyo baada ya vijana kadhaa waliokuwa wakihojiwa na polisi kuitaja.
Vijana hao wanazuiliwa kwa tuhuma za kuhusiana na wapiganaji wa kiisilamu nchini Somalia.
Kundi la Al-Shabab limekuwa likifanya mashambulio kadhaa nchini Kenya kama hatua ya kulipiza kisasi kuwepo wanajeshi wa nchini hiyo Somalia.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List