WAAFRIKA WAONYESHA UWEZO WAO


Issa Hayatou
Rais wa Fifa,S. Blatter, amemthibitisha Issa Hayatou ambaye ni mkuu wa shirikisho la soka la Afrika Caf kama naibu mkuu wa rais wa shirikisho la soka duniani.
Hayati Argentine Julio Grondona,aliyefariki mwezi Julai ndiye alisyeshikilia wadhifa huo.
Ina maana kwamba Hayatou sasa ndiye kiongozi mwanamume wa pili mwenye mamlaka zaidi katika soka duniani.
Blatter alithibitisha wadhifa huo kwa Hayatou ambaye ni raia wa Cameroon, katika mkutano wa hivi karibuni wa kamati kuu ya shirikisho hilo.
Wadhifa wa Hayatou, una maana kuwa yeye ndiye anayewezesha kushikilia wadhifa wa Blatter ikiwa kwa sababu yoyote atashindwa kufanya kazi yake.
Wiki jana shirikisho la Caf pamoja na Hayatou mwenyewe walimuunga mkono Blatter kuwania urais wa shirikisho la FIFA mwaka ujao.
Katika mkutano uliofanyika Ijumaa mjini Zurich, Blatter alikubali kugombea tena urais wa FIFA kwa muhula wa tano.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List