Kampuni ya Tbl imetoa msaada wa kuchimba Kisima cha Maji safi na Salama katika Kituo cha
Afya Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic Kisima hicho kitaghalimu milioni
20 lengo kupunguza shida wanayopata wananchi pindi wanapofika kituo hicho kwa
matibabu na kina mama kwa lengo la kujifungua.
Kituo hicho kimezidi kupanuka kutoa huduma ukilinganisha na
hawali ambapo walikuwa wakitoa huduma kwa akina namama na watoto na hivi ssa hutolewa huduma kwa
jinsia zote kutokana na kuongezeka kwa wakazi wa maeneo hayo kuwa wengi baada
ya majengo kuongezeka ya kuishi watu mbalimbali.
Kituo hicho hivi sasa kinatoa huduma zidi ya watu 500 kwa
siku kwa siku wazazi wanaojifungua 20,huduma kwa wajawazito wapatao 60 .HV wapatao 25,watoto chini ya
miaka 5 wapatao 150 nawengine ni wagonjwa wa magonjwa mbalimbali wakiwepo
jinsia zote.
Afisa uhusiano T.B.L
Doris Malulu amesema baada ya kusikia kilio cha wananchi waishiyo
Mbagala kuwa wanatatizo kubwa la Maji katika kituo hicho kikiwa kikitoa huduma
bora kwa jamii huku akinamama na watoto ndio wameguswa zaidi ndio wenye
mahitaji ya maji wakati wa kujifungua.
Malulu amesema T.B.L imejipanga kusaidia shida ya Maji mikoa yote nchini ambapo imetenga milioni 600
ambazo zitakuwa zikifanya kazi za kusaidia huduma ya maji maeneo ya shule
.Vituo vya Afya na vijijini msaada huu
ulianza kutolewa tangu mwaka huu
ulipoanza na kuhitimisha Desembar mwaka huu.
Mganga Mfaudhi Dr Batuli Luhanda wa Mbagala Roundtable
Matenity Home Clinic amesema msaada huo umefika wakati muwaka kwa kuwa huduma
wameipanua lakini wanakabiliwa na tatizo kubwa la maji baada ya Kisima
kilichopo kushindwa kutoa maji ya kutosha baada ya kukauka vyanzo vya maji
,hali hiyo imechangia kurudisha nyuma hutowaji wa huduma kwa wakati.
Dr Luhanda
amewashukuru Kampuni ya T.B.L kwa
kutoa msaada huo utaweza kuwasaidia kwa kutowa huduma iliyo bora kwa kutumia
maji safi na salama kwa jamii,pia amehaidi kutunza miundombinu hiyo ya maji ili
iweze kutekeleza malengo yaliyokusudia kwa jamii kupata maji salama.
TBL akikabidhi hundi ya fedha kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji kituo cha afya cha Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic
hundi ya fedha kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji kituo cha afya cha Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic
Mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic Dr Batuli Luhanda
Mdau wa maendeleo aliyeshiriki makabidhiano ya hundi.
ENG:ONESMO ZAKANA SIGALLA
Afisa uhusiano T.B.L Doris Malulu
Kituo cha afya cha Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic
TBL akikabidhi hundi ya fedha kwa ajili ya uchimbaji wa kisima cha maji kituo cha afya cha Mbagala Roundtable Matenity Home Clinic
0 comments:
Chapisha Maoni