Manispaa ya Ilala jijini Dar es Salaam imewataka wafanya
Biashara wadogowadogo maharufu kwa jina la machinga waliokuwepo maeneo sio
rasmi katika soko kuu la kari akoo
wafate sheria na taratibu za kufanya biashara kwenye maeneo rasmi lasivyo
hatakayebainika akikiuka taratibu zilizowekwa
hatachukuliwa hatua ya faini ya elfu 50 na mali zake kutahifishwa.
Hayo yamesemwa wakati zoezi la upelesheni wa kusafisha
mazingira manispaa ya Ilala.zoezi limeanza rasmi ambapo wamejikita katika ukamataji
wa machinga wanaofanya biashara maeneo ya Ilala yasiyokuwa rasmi,Usafi wa
mazingira kwa nyumba na viwanda vinavyoelekeza maji taka maeneo yasiyo
rasmi.pamoja na watu wanaojiusisha na vitendo vya uhalifu.
Mkuu wa Idara ya usafi wa mazingira Manispaa ya Ilala
Charles Wambura amewataka Wafanya biashara wote waliopo maeneo ya Ilala wafate
sheria zilizopo ili kuepusha lawama kwa Serikali endapo mtu yoyoyte atakaye bahinika
akikahidi sheria zilizopo.Pia wananchi wameombwa watoe ushirikiano ili zoezi
ilo liweze kufanikiwa.
Mwenyekiti wa zoezi Safisha Manispaa ya Ilala Hassani Mkwawa
pamoja na Afisa Mtendaji Kari akoo Sam Swila wamesema zoezi hilo ni endelevu
kukumbusha wananchi sheria zilizopo kwa kuwa kwa muda mrefu wamekuwa wakikahidi na kujiamulia
wenyewe,Pia zoezi limelenga kuwakamata watumiaji wa madawa ya kulevya
wanaojihusisha na vitendo vya uhalifu walio maeneo hatarishi.
Wamachinga wakiongea na Mwandishi wa Blog wametupia lawama
zoezi hilo la ukamataji ni la unyanyasaji kwa kuwa wapo katika maeneo ya
soko kutokana na kutofanikiwa kumiliki
meza kutokana kuwa chache ukilinganisha na Idadi yao.Hata hivyo wameomba
watengewe maeneo na sio kutaifishwa mali zao na kupigwa faini.
Pamoja na zoezi hilo la Safisha Manispaa ya Ilala kwa hali
ya mazingira bado ni mbaya na mfumo wa maji taka ni wazamani haukizdhi mahitaji ya hivi sasa kwa wakazi wa
manispaa ya Ilala.kutokana hongezeko kubwa la idadi ya Wakazi wa Kariakoo baada
ya kujengwa kwa majengo ya ghorofa wakati miundombinu ya Majitaka bado ni ya zamani na haitoshelezi mahitaji huku
ikiwa chakavu.
Bodaboda na biashara zilizokamatwa katika zoezi la weka manispaa safi.
Bodaboda na biashara zilizokamatwa katika zoezi la weka manispaa safi.
Mkuu wa Idara ya usafi wa mazingira Manispaa ya Ilala Charles Wambura
Mwenyekiti wa zoezi Safisha Manispaa ya Ilala Hassani Mkwawa
Lenatusi Ruhungu afisa mtendaji kivukoni.
Bodaboda na biashara zilizokamatwa katika zoezi la weka manispaa safi.
wafanya biashara nje ya soko karia koo wakifanya biashara kwa wasiwasi kutokana na zoezi la ukamataji wa machinga.
Miundombinu mibovu ya maeneo ya karia koo ambapo Manispaa ya Ilala wametaka kuweka safi.
Bodaboda na biashara zilizokamatwa katika zoezi la weka manispaa safi.
wafanya biashara nje ya soko karia koo wakifanya biashara kwa wasiwasi kutokana na zoezi la ukamataji wa machinga.
wafanya biashara nje ya soko karia koo wakifanya biashara kwa wasiwasi kutokana na zoezi la ukamataji wa machinga.
Afisa Mtendaji Karia koo Sam Swila
0 comments:
Chapisha Maoni