Jumuiya ya wazazi ya CCM,Wilaya ya Kinondoni,Imesema
maandamano pekee yanayopangwa kufanywa na baadhi ya vyama vya upinzani,vilivyo
chini ya Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA),Hayawezi kuwa suluhisho la
mabadiliko,bali yanaweza kuwa chachu ya kuhatarisha Amani na Umoja uliopo
nchini.
Haya yameelezwa katika ufungaji wa Semina elekezi ya Jumuiya
ya Wazazi wilaya ya Kinondoni iliyoshirikisha majimbo yake matatu ya
kinondoni,Kawe na Ubungo.
Kwenye Semina hiyo elekezi,wanajumuiya hawa wamejipanga
namna ambayo watahakikisha chaguzi zinazokuja zinatakiwa kuwa na mafanikio na
jinsi ambavyo wamefanikiwa kutekeleza Ilani ya Chama cha mapinduzi.
Aidha,wanatumia hadhara hii kuonya kuhusiana na maandamano
yanayotarajiwa kufanyika nchi nzima hivi karibuni Ili kushinikiza Kuahirishwa kwa
Bunge maalumu la KATIBA.
Katibu wa jumuiya hiyo wilaya ya kinondni Ephraim Kolimba
amesema kinachofanyika hivi sasa ndani ya chama ni kurejesha heshima yake.kwa
kufuata kwa Umakini nyayo za mwasisi wake Hayati Mwalimu Julius Nyerere
Baadhi ya viongozi wa jumuiya ya wazazi walioshiriki Semina
hiyo walikuwa na maoni haya baada ya kuhudhuria Semina hiyo.
Pamoja na mambo hayo CCM imejipanga kurudisha mitaa mitano 5
na kata sita 6zilizochukuliwa na wapinzani kwa kuweka wagombea wanaokubalika na
wananchi.
Mh:Lucas Mgonja(Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi,Kinondoni)
Justins Sangu(Mwenyekiti wa wazazi jimbo la ubungo)
Katibu wazazi wilaya kinondoni Ephraim Kolimba
Mwajuma Mlungira katibu wa wazazi jimbo la Ubungo.
Mh:Lucas Mgonja(Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi,Kinondoni)
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
Meza kuu siku ya kufunga semina hiyo elekezi kwa jumuiya ya wazazi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki wafungaji wa semina hiyo Elekezi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
Wana CCm wa jumuiya ya wazazi walioshiriki ufungaji wa semina hiyo Elekezi.
0 comments:
Chapisha Maoni