Imeelezwa kuwa mchakato wa kuiweka Misitu ya safu ya Milima ya Tao la mashariki katika urithi wa Dunia ili kulinda viumbe Hadimu vilivyogunduliwa Tanzania hivi karibuni ambavyo viko mbioni kutoweka huenda usifanikiwe kutokana na kuwepo kwa uharibifu mkubwa wa Mazingira katika misitu hiyo.
Mchakato huo ambao awali ulikuwa ufanyike na baadae Serikali kuamua kuufuta unaendelea huku ukiwa na lengo la kulinda na kuhifadhi misitu hiyo.
Mkurugenzi wa shirika la Hifadhi Misitu ya asili Tanzania Charles Meshack anaiomba Serikali kupititia upya mchakato huo ili uweze kuwa na manufaa kwa Taifa kutokana na kukuza utalii ambao unaliingizia Pato taifa.
Mbali na kuliingizia Taifa Pato la kigeni lakini Misitu hiyo pia inatajwa kuondoa Hewa ukaa inayozalishwa viwandani ambayo uathili viumbe hai vilivyopo nchini.
Aidha katika suala la uhifadhi Misitu pia Serikali nayo ikashauriwa kutoa Elimu kwa wakazi waishio Jirani na Misitu Hiyo ili kuweza kuepukana na Uharibifu wa mazingira.
Inaelezwa kuwa Bado kuna Tatizo kubwa la Uelewa kuhusiana na utunzaji wa Mazingira Hali ambayo inatajwa kuhatarisha kutoweka kwa baadhi ya viumbe hai nchini hali ambayo wataalamu wanasema ipo haja ya kufanya mikakati mbadala ya kunusuru misitu Hiyo.
Moja ya Misitu ya asili yenye kivutio kikubwa nchini Tanzania.
Baadhi ya viumbe wazuri aina ya chura wanaopatikana Tanzania.
Moja ya Misitu ya asili yenye kivutio kikubwa nchini Tanzania.
Baadhi ya viumbe wazuri aina ya kinyonga wanaopatikana Tanzania.
Mkurugenzi wa Hifadhi misitu ya Asili Tanzania Ndugu: Charles Meshack
Elinasi Monga(Meneja Mradi toka Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania)
Gerald kitabu (Mwenyekiti Jukwaa la Waandishi habari Kilimo Tanzania)
0 comments:
Chapisha Maoni