Watuhumiwa wafanya Biashara haramu wa dawa za kulevya wakamatwa na kilo saba za Dawa za Kulevya aina ya Heroin,zinazodhaniwa kuwa na thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 300 usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Watu hao wamekamatwa maeneo ya Magomeni jijini Dar es Salaam,usiku wa kuamkia Jumanne hii.
Wafanyabiashara wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi Kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya watuhumiwa hao ni Mwalami Mohamed Chonji,Mariki Zuberi,Taka Adam,Rehan Musso na Abdul Abdallah ambao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.
Kamishina msaidizi Mwandamizi wa Kitengo hicho,Godfrey Nzowa amesema,kukamatwa kwa watu hao kunafuatia taarifa kutoka kwa raia wema waliowatilia shaka watu hao.
Aidha,kamishna Nzowa ameendelea kuwataka wananchi kuachana na Biashara hiyo haramu,ikiwa ni pamoja na kutoa wito kwa wakulima wanaozalisha zao la bangi kuacha mara moja ,kwa kuwa zao hilo ni miongoni mwa dawa za kulevya.Zaidi ya kilo mia tatu za Heroin zimekamatwa na kitengo hicho tangu kuanza kwa mwaka huu.Hali hiyo inayopunguza kasi ya biashara hiyo hapa nchini.
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya madawa yaliyokamatwa.
Baadhi ya Dawa za kulevya zilizowahi kukamatwa na GODFREY NZOWA
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya)
Dawa za kulevya zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300
Dawa za kulevya zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300
Mizani iliyokuwa inatumika kupimia Dawa za kulevya.
Kifaa kimojawapo ambacho wamekamatwa nacho watuhumiwa hao wa Dawa za Kulevya.
Dawa za kulevya zilizokamatwa leo Magomeni aina ya Heroin kilo saba zenye thamani ya shilingi Bilioni 300
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya dawa za kulevya yaliyokamatwa.
GODFREY NZOWA(Kamishina msaidizi Mwandamizi kitengo cha kudhibiti na kupambana na Dawa za kulevya) akionyesha baadhi ya dawa za kulevya yaliyokamatwa.
0 comments:
Chapisha Maoni