JE MANGAPI MUHIMU TUNAYAENZI TOKA KWA BABA WA TAIFA MW.JULIUS KAMBARAGE NYERERE?

Tumekuwa tukifanya  maadhimisho ya siku ya Mw.Julius Kambarage Nyerere kila 14 mwezi wa 10 ila kuna mambo mengi ambayo binafsi aliyajangea msingi lakini tunashindwa kuyafuata kama sehemu ya kumbukumbu ya Mw.Nyerere.Wakati wa uhai alisisitiza sana Muungano hasa uliokuwepo wa Serikali mbili kwa mfumo wa pekee japo maisha ya Binadamu yanabadirika lakini Hakukubali kabisa kufanya Mgawanyo wa Serikali zaidi Mbili ni jambo ambalo aliliongelea sana,Zaidi pia aligusia viongozi wenye uroho wa Madaraka na wanao chukua rushwa kwa wananchi kwamba ni viongozi ambao wakupigwa vita kama Ukoma na Kusisitiza kumwogopa mtu anayetaka kwa nguvu madaraka.

Alipigana vita dhidi ya Ujinga,Maradhi na Rushwa ambapo sasa tatizo la rushwa linaonekana kuongezeka richa ya Serikali kuchukua hatua za ziada kukabiliana na tatizo hilo.Katika Maisha yake alitamani sana kuona Watanzania wanapata Elimu inayoweza kumfanya mtu ajipatie ajila mwenyewe(self reliance education) na kusisitiza Taifa litakaloweza kujitegemea lenyewe.

Kuna Mengi aliyafanya na kusema mazuri je Mangapi muhimu tumeyachukua toka kwake.Mwalimu Julius Kambarage Nyerere atakumbukwa Daima.




Share on Google Plus

About SDM PRODUCTION MEDIA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List