Idadi ya vifo vya majeruhi
walioungua moto kutokana na ajali ya moto iliyotokea Mbagara Jijini Dar
es salaam,Usiku wa kuamkia Jumanne hii imeongezeka na kufikia watu 4 Huku hali
za majeruhi wengine 11 waliolazwa hospitali ya taifa Muhimbili zikielezwa kuwa
si za kulizisha.
Majeruhi waliofikishwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada
ya Kuhamishiwa kutoka Hospitali ya
Temeke walikuwa 15 na hadi sasa ni majeruhi 11 tu ndo wanaendelea kupata matibabu.
Majeruhi hao 11 wamerazwa kwenye wodi 23 ya sewahaji maalum
kwa ajili ya majeruhi walioungua huku uongozi wa Hospitali ukikili kuwa kwa
Hali za majeruhi hao ambao wengi wameungua kwa zaidi ya asilimia 40 ya miili
yao ikiwa si ya kulizisha.
Doris Ishenda (afisa uhusiano MNH) amewaonya baadhi ya
wananchi kuhusiana na matukio kama hayo ambacho wananchi hukimbilia eneo la
ajali ili kupata chochote.
Bado hakuna taarifa ya kuwepo kwa vifo vingine vilivyotokea
nje ya Hospitali kutokana na ajali hiyo ya Moto.
Doris Ishenda (afisa uhusiano MNH)
Doris Ishenda (afisa uhusiano MNH)
Wahanga wa ajali hiyo ya moto ya roli lililopata ajali.
Wahanga wa ajali hiyo ya moto ya roli lililopata ajali.
Wahanga wa ajali hiyo ya moto ya roli lililopata ajali.
Wauguzi wakiendelea kutoa huduma kwa wahanga wa ajali hiyo.
0 comments:
Chapisha Maoni