Wakati mfuko wa Bima
ya Afya wa Taifa,NHIF ukiongeza jitihada za kukabiliana na changamoto za
upungufu na dawa na vifaa tiba,changamoto nyingine ya kutokuwepo kwa motisha ya
wataalamu wa Tiba kunaweza kuchangia
kuondoa ari ya wataalamu hao kiutendaji.
Hali hii,iwapo haitadhibitiwa inaweza kuathiri utoaji wa
Huduma,Hata kama kutakuwepo na vifaa vya kutosha kwenye vituo vya huduma za
afya.
Mfuko wa Bima ya afya,umekuwa ukiongeza huduma
zinazowesha upatikanaji wa tiba kuwa
rahisi zaidi kwa kila mwanannchi ingawa changamoto hii,Ya motisha inatajwa kuwa
kikwazo kingine kwenye utendaji.
Serikali inaombwa kulinganisha ili kwa namna ya kipekee ili
kuwawezesha wataalamu wa tiba kujituma zaidi huku NHIF yenyewe ikivitaka vituo
vya tiba kuhakikisha vinatumia vyema Huduma zake katika kujiongezea dawa na
vifaa Tiba .
Dr Frank Lekei
(Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF)Ameyasema alipokuwa akitoa
msaada wa mashuka 150 toka NHIF
hospitali ya vijibweni iliyokuwa ikikabiliwa na upungufu wa mashuka kwa kipindi
cha miezi mnne sasa.
Dr Emmanuel Bwana(Mgaga Mfawidhi hospitali ya vijibweni),Changamoto
bado inatolewa kwa wananchi kujiung na mfuko wa Bima ya afya wenye Huduma
mbalimbali ili kujihakikishia uwezekano wa kupata Huduma,Kwa kipindi chochote
cha ugonjwa.
Hospitali hiyo inayopokea wagonjwa 450 hadi 500 kwa siku
unakabiliwa pia na upungufu mkubwa wa Dawa na vifaa Tiba hivyo kuomba wahisani
kuendelea kuisaidia ili kunusuru kaya nyingi zinazotegemea huduma zake.
Waaguzi na Waganga wa hospitali ya vijibweni wakionyesha mashuka ambayo wamepatiwa na shirika la NHIF
Waaguzi na Waganga wa hospitali ya vijibweni wakionyesha mashuka ambayo wamepatiwa na shirika la NHIF
Diwani wa kata ya Vijibweni Mh:Suleiman Matthew
Dr Emmanuel Bwana(Mgaga Mfawidhi hospitali ya vijibweni)
Mgonjwa anayepatiwa matibabu katika Hospitali ya Vijibweni.
Dr Frank Lekei (Mkurugenzi wa Tiba na masuala ya kiufundi NHIF)
Juma Mkenga(Naibu Meya-Temeke)
Viongozi wa Serikali,Wauguzi,Waganga na Wataalamu toka NHIF wakati wa makabidhiano wa msaada mashuka ndani ya Hospitali ya Vijibweni.
Viongozi wa Serikali,Wauguzi,Waganga na Wataalamu toka NHIF wakati wa makabidhiano wa msaada mashuka ndani ya Hospitali ya Vijibweni.
0 comments:
Chapisha Maoni