Jamii nchini
wenye uwezo wa Kipato wameshauriwa kujitolea kusaidia Sekta ya
Afya,inakabiliwa na matatizo mengi aswa katika upande wa huduma ya akina mama
na Mtoto changamoto kubwa ukosefu wa vifaa vya huduma vya uzazi kwa akina mama.na sio kuachia kila
jambo kufanya serikali pekee.
Hayo yameelezwa katika Kituo cha Afya cha Majohe Dispensary
iliyopo wilaya ya Ilala jijini Dar Es salaam baada ya kupokea msaada wa Kitanda
cha Kuzalishiwa akinamama wajawazito kimeghalimu milioni moja na laki
tano,msaada huo umetolewa na Kanisa la
Calvary Ass of God Majohe Mikanjuni chini ya usimamizi wa Mch,Nabii Amos
Peter Lilai.
Nabii Amos Lilai amesema wameamuwa kutoa msaada kwa wanahoitaji
kwa kuwa ndio mpango wa Mungu kusaidia eneo lenye uwitaji ilikutekeleza
maandiko Matakatifu,amesema kwakuwa walipata hufahamu kituo hicho kinahukosefu
wa Kitanda cha kuzalishia akina mama ndipo walipoguswa na kuona humuimu wa
kutoa msaa wa Kitanda cha kuzalishia akinana,lengo kuhepusha vifo
visivyotalajia wakati wa kujifungua ili waachane na kulala chini kutokana na
hukosefu wa kitanda kimoja.
Dr Elias Mbao wa Majohe Dispensary amesema msaada uliotolewa
umefika wakati muwafaka kwa kuwa wanakabiliwa na hupungufu wa Kitanda Kimoja
,kulingana na mahitaji ya hongezeko la huduma za akina mama na mtoto,hatavhivyo
walipeleka maombi ya kuongezewa Kitanda kimoja serikalini hivi sasa ni muda
mrefu waliambiwa ombi ilo linafanyiwa kazi,ameshukuru kwa Kanisa ilo kutoa
msaada huo,hata hivyo ametowa wito kwa watu wengine nao waweze kujitoleya waige
mfano wa Kanisa la Calvary Ass of God
Majohe.
Naye mwnyekiti wa akinamama kanisa hilo la Calvary Ass of God Majohe bi
Catherine Massaga ametowa wito kwa Wahuguzi msaada uliotolewa wa Kitanda
waangalie na kukitunza vizuri ili kiweze
kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa
kutumia wagonjwa walio wengi huduma ya Kitanda hicho.
Serikali pamoja na jitihada zake kubwa kuboresha sekta ya
Afya nchini lakini bado kunachangamoto zinzojitokeza za hupungufu wa Vifaa
katika vituo vya Afya nchini,kila mmoja anatakiwa kuguswa na tatizo la Afya na
sio kuachia serikali pekee ,hata hivyo msaada huo uliotolewa ulienda sambamba
na zoezi la usafi wa Mazingira wa kituo cha afya hicho ,huduma hiyo iliweza
kutolewa na Wahumini wa Kanisa la Calva Ass of God Majohe wakishirikiana na
Nabii Lilai hilo pia waliweza kuwafariji wagonjwa wote waliokuwepo siku hiyo
wakienda sambamba Ibada maarum ya Maombezi.
Kitanda cha kisasa kilichotolewa msaada na Kanisa la Calvary Ass of God Majohe Mikanjuni chini ya usimamizi wa Mch,Nabii Amos Peter Lilai.
Dr.Elias Mbao wa Majohe Dispensary.
RBECCA J.MBOYA(Nurse incharge)
wakati wa makabidhiano wa kitanda cha kisasa kwa ajili ya kuzalishia wakina Mama watumiaji wa Majohe Dispensary.
Mchungaji na Nabii Amos Peter Lilai.
Dr Elias Mbao wa Majohe Dispensary akihojiwa na waandishi wa Habari.
Catherine Massanga(mwenyekiti wa kinamama CAG majohe)
Jengo la Majohe Dispensary
wakifanya makabidhiano ya kitanda cha kisasa kwa ajili ya kujifungulia wakinamama.
Wananchi na Waumini walioshiriki siku ya Makabidhiano.
0 comments:
Chapisha Maoni