Mfumo wa fedha wa sasa uliopo nchini unatajwa kuwa
miongoni mwa vikwazo vinavyosababisha
wawekezaji wa ndani kushindwa kupata mikopo pamoja na huduma kutoka kwenye
taasisi za fedha hivyo wengi kushindwa kuwekeza kutokana na kuwa na mitaji midogo.
Baadhi ya wawekezaji wenye mitaji ya kati,wameshindwa kuwekeza
hasa kwenye miradi mikubwa ya sekta ya nishati,hivyo miradi mingi kuchukuliwa
na wawekezaji wan je.
Ni mionguni mwa wawekezaji wanaokutanishwa na mpango huu wa
kuwawezesha wawekezaji wa miradi mikubwa na midogo kwenye maeneo ya ufundi na
fedha ili kuwasaidia kupata na kuendesha miradi yao wenyewe.
Kwa ushirikiano na Serikali kupitia wizara ya TAMISEMI
taasisi ya umoja wa mataifa ya UNCDF ,imekuwa ikiwakutanisha wadau hao wa
maendeleo ili kuangalia namna watakavyowawezesha kupata huduma hizo muhimu
katika kuboresha miradi yao.
Hata hivyo bado kuna changamoto za kiutendaji kwa wawekezaji
hao katika kujihakikishia wanapata misaada hiyo
Mpango huo pamoja na uwezeshaji unalenga kuhakikisha kuwa
uwekezaji kwenye miundombinu hususan ya maeneo ya vijijini unaboreshwa ili
kusogeza huduma nyingi zaidi kwenye maeneo hayo ambazo kwa sasa zinapatikana
zaidi mijini
UNCDF unataraji
kuendelea kutoa huduma zake nchini hadi mwaka 2017 ambapo itaanza
kusambaza huduma zake kwenye nchi nyingine Barani Afrka
Wadau wa Maendeleo walioshiriki mkutano wa kupeana maarifa juu ya namna ya kukuza maendeleo.

PETER MALIKA(Chief Technical Advisor)
JUMA .S. SHAMTE(Director of Development)
Wadau wa Maendeleo walioshiriki mkutano wa kupeana maarifa juu ya namna ya kukuza maendeleo.
0 comments:
Chapisha Maoni