Imeelezwa kuwa mchakato wakuiweka Misitu ya safu ya Milima ya
Tao la mashariki katika urithi wa Dunia ili kulinda viumbe Hadimu
vilivyogundiwa Tanzania hivi karibuni ambavyo viko mbioni kutoweka huend usifanikiwe kwa kutokana na kuwepo kwa
haribifu mkubwa wa Mazingira katika misitu hiyo.
Mchakato huo ambao awali ulikuwa ufanyike na baadae Serikali
kuamua kuufuta unaendelea ukiwa na lengo la kulinda na kuhifadhi misitu hiyo.
Mkurugenzi wa shirika
la Hifadhi Misitu ya asili Tanzania Charles Meshack anaiomba Serikali kupititia
upya mchakato huo ili uweze kuwa na manufaa kwa Taifa kutokana na kukuza utalii
ambao unaliingizia Pato taifa.
Mbali na kuliingizia Taifa Pato la kigeni lakini Misitu hiyo
pia inatajwa kuondoa Hewa ukaa inayozalishwa viwandani ambayo uathili viumbe
hai vilivyopo nchini.
Aidha katika suala la uhifadhi Misitu pia Serikali nayo
ikashauriwa kutoa Elimu kwa wakazi waishio Jirani na Misitu Hiyo ili kuweza kuepukana na Uharibifu wa mazingira.
Inaelezwa kuwa Bado
kuna Tatizo kubwa la Uelewa kuhusiana na utunzaji wa Mazingira Hali ambayo
inatajwa kuhatarisha kutoweka kwa baadhi
ya viumbe hai nchini hali ambayo wataalamu wanasema ipo haja ya kufanya
mikakati mbadala ya kunusuru misitu Hiyo.
Moja ya Misitu ya asili yenye kivutio kikubwa nchini Tanzania.
Baadhi ya viumbe wazuri aina ya chura wanaopatikana Tanzania.
Moja ya Misitu ya asili yenye kivutio kikubwa nchini Tanzania.
Baadhi ya viumbe wazuri aina ya kinyonga wanaopatikana Tanzania.
Mkurugenzi wa Hifadhi misitu ya Asili Tanzania Ndugu: Charles Meshack
Elinasi Monga(Meneja Mradi toka Shirika la kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania)
Gerald kitabu (Mwenyekiti Jukwaa la Waandishi habari Kilimo Tanzania)
0 comments:
Chapisha Maoni