Jamii nchini imeshauriwa kutowanyanyapaa waathirika wa dawa
za kulevya nchini kwa kuwa nao ni Wagonjwa kama wagonjwa wengine ingawa huwa na
athari za Kisakolojia,kudhoofu Afya ya mwili ,kupoteza mwelekeo wa maisha
lakini pia wana Haki sawa kama binadamu wengine.
Wananchi wameombwa kuunga mkono suala la kudhibiti Biashara
ya Dawa za kulevya ili kuokoa vijana wanaoteketea kutokana na kutumi Dawa hizo
kwani wao ndio nguvu kazi ya Taifa.Akiongezea amesema tatizo la Dawa za kulevya
ni la Dunia zima,na Nguvu ya pamoja ndo inaweza kusaidia Mataifa Mbalimbali
kupiga Vita Uingizaji wa DAWA ZA KULEVYA pamoja na matumizi yake.Hayo
yalizungumzwa na AFISA TAWALA MKUU TUME YA KURATIBU DAWA ZA KULEVYA Bi:AIDA
TESHA.
SHIRIKA LA KIMATAIFA LA COMMUNITY ANT.DRUG COALITIONS OF
AMERICA(CADCA),limesema uwepo wake Tanzania utasaidia kuongeza nguvu katika
kupamabana na Dawa za kulevya kwa kutolewa elimu kwa jamii.CADCA wamesema
watatumia njia ya kujenga makubaliano kwa jamii(community coalition)na
kumshirikisha kila mtu kwa kuipa nguvu na uamuzi jinsi ya kupambana na Dawa za
kulevya.
Tanzania mikoa inayoongoza kwa kuwa na waathirika wa Dawa za
kulevya ni pamoja na Dar es salaam,Pwani,Tanga,Mtwara,Morogoro na Arusha.CADCA itashirikiana
na SDM PRODUCTION MEDIA kwa kupitia YFSO(Youth friend service) na taasisi ya
T-IOGT(Tanzania International organization of good Tamplars) Pomoja na Tume ya kudhibiti Dawa za Kulevya Tanzania.
AFISA TAWALA MKUU TUME YA KURATIBU DAWA ZA KULEVYA Bi:AIDA TESHA.
ERIC SIERVO,M.ED.(Senior Manager CADCA)
COLBER PROSPER(SENIOR CONSULTANT PROSPER &PARTNERS)
CADCA TEAM baada ya Kikao.
Wadau wa kupambana dhidi ya Dawa za kulevya wakipeana Mkono baada ya kikao.
Picha ya Pamoja baada ya kumaliza kikao.
Picha ya Pamoja baada ya kumaliza kikao.
0 comments:
Chapisha Maoni