Makamamu wa Rais Dkt Ghalib Bilali amewataka viongozi wa
chama cha mapinduzi-CCM ngazi ya wilaya na mkoa kuhakikisha wanakuwa makini
katika uteuzi wa kuraa za maoni na kuhakikisha mgombea anayeteuliwa anakubalika
ndani ya jamii.
Dkt Balali ametoa tahadhali hiyo ikiwa ni siku 30 tu
zimesalia kuanza kwa harakati za uchaguzi wa serikali za mitaa unaotarajia
kufanyika Desemba 14 mwaka huu.
Amesema katika Uchaguzi wa mwaka 2009/10 katika Mchakato wa
Kura za Maoni zilijitokeza Kasoro zilizotokana na uchaguzi wa Wagombea
wasiokubalika na Jamii, Hali iliyopelekea CCM kupoteza nafasi zake nyingi na
hivyo kuchukuliwa na upinzani
Dkt Bilali amesema nia ya Chama cha mapinduzi ni kuhakikisha
wanapata ushindi wa kishindo hivyo akawataka Viongozi wa CCM kuhakikisha
wanaepuka Malalamiko katika uteuzi wa kura za maoni na kuyafanyia kazi
Akifungua mkutano Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dar es salaam,
uliyojadili namna ya kushiriki kwenye chaguzi za serikali za mitaa, Dkt Bilali
ambaye pia ni mlezi wa Mkoa huo kichama amesema silaha kubwa ya ushindi ni
kuchagua mgombea anayekubali.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mkoa wa Dar es Salaam, CCM
Ramadhan Madabida akatoa msimamo wa chama hicho katika kuhakikisha kasoro hizo
hakizijitokezi.
Hadi sasa tayari wagombea 2519 wamejitokeza kugombe nafasi
mbalimbali za uongozi katika chaguzi za serikali za mitaa na kwa mujibu wa CCM Mkoa wa Dar es salaam,
Novemba 16 hadi 17 ndiyo siku ya kuanza uteuzi wa kura za maoni kwa wagombea
kupitia chama hicho.
0 comments:
Chapisha Maoni