Wasichana waishio katika mazingira hatarishi wamepatiwa
mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali ikiwemo ufundi ushonaji ili kuwasaida waweze
kujipatia kipato
na kuachana na tabia hatarishi ya kujipatia kipato kwa kufanya
ngonozembe .
Mafunzo hayo yametolewa bure na Asasi ya Chagua Maisha iliyopo Jijini Dar Es
Salaam kwa wasichana zaidi 165 wanaoishi kwenye mazingira hatarishi kutoka
Yombo,Mbagala na Chanika Jijini Dar Es Salaam kwa lengo la kubadili maisha
yao Kiuchumi na kimaadili ili wawe mfano kwa jamii
Miongoni mwa kumbukumbu mbaya ambazo zitaendelea kubaki
vichwani mwa wanawake wengi waliotumbukia katika biashara ya uuzaji miili yao
Eneo la uwanja wa fisi lililopo katikati ya jiji la Dar es
Salaam maarufu kwa biashara ya ukahaba. Hili ni miongoni mwa madangulo mengi
yaliyotapakaa sehemu mbalimbali nchini ambapo kila aina ya uhalifu unafanyika
hapa tena hadharani na kwa wakazi wa eneo hili kwao ni matukio ya kawaida
kabisa.
Huenda changamoto za ugumu wa maisha ndizo zinazopelekea
vijana wengi haswa wasichana kukata tamaa na kuamua kujiingiza kwenye biashara
ya uuzaji miili yao wakiamini huenda wakapata ahueni ya kimaisha na kujikwamua
kiuchumi ili waweze kujikimu walau kwa mahitaji yao madogomadogo ya kila siku
ndoto ambayo inabaki kuwa kiza kinene kwa walio wengi kwani badala yake
huambulia magonjwa mbalimbali ya ngono ikiwemo maambukizi ya virusi vya Ukimwi
Na sasa wapo wanaojutia ingawa kwao matumaini yamerejea
baada ya kusaidiwa kutoka katika sehemu hizo hatarishi na wameamua kuanza
maisha mapya huku wakiwataka wenzao pia wajitokeze hadharani ili wapatiwe
msaada.
Bi Johari Sadick yeye ni mlezi wa wanawake hawa.
Wasichana wa kike zaidi ya 165 waliojitokeza hadharani wanapatiwa msaada wa
mafunzo ya kiujasiliamali katika kituo hiki kipya cha ufundi kushona na
wanapatiwa pia elimu ya vvu na ukimwi ili wasiweze tena kurudi katika biashara
hiyo huku wito ukitolewa kwa vijana wengi zaidi kujiepusha na makundi hatarishi
0 comments:
Chapisha Maoni