Serikali haitaweza
kuboresha sekta ya elimu nchini kutokana na kukabiliwa na majukumu mengi,hivyo
imetakiwa Jamii kushirikiana kwa pamoja kutoa michango ya kuongezea nguvu ya
dhiada ili kuboresha elimu
Imeelezwa wananchi waachane na tabia ya kutoa michango
mikubwa katika sherehe za Arusi na Ngoma,na badala yake wawekeze katika maswala
ya elimu itakayo weza kusaidia kupata wataalam wa ndani haswa wa Sayansi, hayo yameelezwa Jiji Dar Es
Salaam ambapo waliweza kupewa Vyeti kwa
waliosaidia kutoa michango katika Sekta ya Elimu.
Prof Emanual Bavu
amesema serikali inamzigo mkubwa wa Majukumu ,ambapo sekta ya elimu inamahitaji
mengi kwa kuachia serikali pekee taifa alitaweza kufanikiwa sekta ya Elimu
Naye Naibu Waziri wa Elimu na mafunzo ya Ufundi Mhe Jenista
Mhagama ametowa wito kwa Watanzania
kubadilika kuwekeza katika sekta ya Elimu waachane na tabia ya kutoa michango
mikubwa katika sheree za Arusi na Ngoma.
Baadhi ya Wadau wa Elimu waliotunikiwa Vyati kutoka sekta
Binafsi na Serikali walikuwa na haya ya kusema
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali taifa
litafanikiwa kutoa elimu bora na sio bora Elimu
0 comments:
Chapisha Maoni