Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye
thamani ya zaidi ya shhilingi milioni
arobaini kwa ajili ya kusaidia maendeleo katika jamii.
Vifaa vilivyotolewa ni madawati 100 kwa shule ya
msingi Misitu iliyopo kata ya kivule pamoja na vifaa vya usafi katika hospitali
ya wilaya ya Temeke.
Kaimu Kamishna Mkuu wa forodha TRA Tiagi Masamaki
amesema TRA imetoa msaada huo ikiwa ni muendelezo wa kuadhimisha wiki ya mlipa kodi.
Naye Muuguzi wa wagonjwa waliolazwa katika Hospitali
hiyo Nurse Nuswe Ambokile amesema msaada huo umekuja wakati muafaka
Mwalimu Mkuu wa shule ya msingi Misitu Bi Hyasinta Hugo amesema kumekuwa na changamoto nyingi
katika sekta ya Elimu nchini.
Diwani Kata ya
Kivule Nyansika Motena na baadhi ya wanafunzi
wa shule hiyo wamezungumzia msaada huo.
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA inatarajia kuhitimisha
ziara zake za wiki ya mlipakodi katika visiwa
vya Zanzibar ambapo pia watafanya shughuli za kijamii.
0 comments:
Chapisha Maoni