TASWA YAOMBOLEZA VIFO VYA WANACHAMA WAKE, MUNYUKU NA KARASHANI



Habari wadau, kwa masikitiko makubwa nawajulisha kuwa mwanachama mwenzetu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Baraka Karashani amefariki dunia mchana huu katika hospitali ya jeshi Lugalo alikokuwa amelazwa akipatiwa matibabu.  
Pia mwandishi mahiri wa zamani wa habari za michezo nchini Innocent Munyuku, naye amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Hilo ni pigo kwa waandishi wa habari za michezo na wanamichezo kwa ujumla, maana wote wameondoka wakati bado mchango wao ukihitajika sana. Taarifa zaidi tutaendelea kupeana kwa njia mbalimbali. Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi. Amina.

Nawasilisha,
Amir Mhando
Katibu Mkuu TASWA
19/11/2014
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List