Waziri Kiongozi
mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Shamshi Vuai Nahondha amesema
Serikali inakusudia kuanzisha Sheria mpya ya kodi itakayokuwa na msukumo rafiki
kwa wafanyabiashara kuwa na utamaduni wa kulipa kodi kwa hiari na wakati.
Akizungumza kwenye Maadhimisho ya Siku ya mlipa kodi Jijini
Dar Es salaam, Nahodha, amesema uanzishwaji wa sheria hiyo ni mpango Mkakati wa
Serikali kutaka Nchi iwe na mfumo mmoja wa ukusanyaji kodi.
Amesema sheria iliyopo sasa ya ukusanyaji kodi imetoa mwanya
mpana wa kuruhusu kuwa na kodi nyingi ambazo zimesababisha walipa kodi wengi
kutokuwa rafiki wa ulipaaji kodi kama ilivyo kwa nchi zilizoendelea.
Kwa kutambua hilo hivi sasa nchi imeweka misingi imara ya
ukusanyaji kodi kwa kuwa na mfumo mmoja utakahusisha maeneo yote ya ukusanyaji
ikiwemo serikali kuu na halmshauri.
Kwa upande wake Naibu waziri wa Fedha Adam Malima amesem nia
ya serikali ni kuona Nchi inakuwa na uchumi mzuri unaotokana na ulipaji kodi za
ndani lakini mafanikio yake bado yanachangamoto
Novemba 21 kila mwaka ni siku ya mlipa kodi, Mamlaka ya
mapato nchini ndiyo wenye dhamana na siku hiyo, Rished Bade ni Kamshina Mkuu wa
TRA,mpango wa mamlaka yake kuanza kutumia mfumo wa Teknohama kama njia mkakati
ya kuwa na makusanyo mazuri.
Maadhimisho hayo ni ya nane kufanyika na kwa kupitia siku ya
mlipa kodi Serikali imeweka lengo kuhakikisha inakusanya Mapato yatokanayo na
Kodi yanafikia shs Trioni 11.9 kwa mwaka wa fedha 2014/15 mwisho
0 comments:
Chapisha Maoni