WASOMAJI na
wadau wangu nawasalimu na naimani kuwa Mwenyezi Mungu ametujalia
tumeuona mwaka mpya wa 2015 salama salmini. Nawatakia heri na fanaka
katika mwaka huu pia na karibuni tena katika porojo zangu za ukweli.
IDARA
ya Habari –MAELEZO ndiyo idara ya serikali inayoshughulika na kufanya
kazi zake kama chombo cha usimamizi wa vyombo vya habari na waandishi
wake.
Idara hiyo
pia ndio msemaji wa masuala mbalimbali ya serikali lakini pia ndiyo
idara yenye jukumu la kusajili au hata kuyafutia usajili magazeti hapa
nchini na vyombo mbali mbali vya hjabari.
Waandishi wa
habari waajiriwa na wale wa kujitegemea wameanza mchakato wa kujaza
fomu kwaajili ya kupatiwa vitambulisho vipya vya kazi (PRESS CARD) kwa
mwaka 2015.
Jambo hili
ni zuri kwa waandishi wa habari maana kitambulisho hicho cha
serikali hutolewa kwa waandishi walio na sifa za uandishi tu na sio wale
waparamia fani za watu maarufu kama kanjanja.
Ndio!
Uandishi wa habari ni taaluma kama taaluma nyingine, kwa hiyo kila
mwanahabari anatakiwa kuwa na Press Card ambacho ndicho kitambulisho cha
serikali, kama huna basi wewe sio muandishi au laa hujakomaa kuwa
muandishi. SOMA ZAIDI FATHER KIDEVU BLOG
0 comments:
Chapisha Maoni