NGUMI KUPIGWA FEB 28 UWANJA WA NDANI WA TAIFA



Na Mwandishi Wetu
MPAMBANO wa masumbwi unaosubiliwa kwa hamu kubwa na washabiki mbalimbali wa mchezo wa masumbwi nchini kwa sasa ni kati ya bingwa wa WPBF Africa Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Cosmas Cheka ambao watagombania ubingwa wa U.B.O Africa siku ya Feb 28 katika uwanja wa ndani wa Taifa 'Indoor Stadium' pia siku hiyo kutakuwa na mpambano mwingine wa mahasim wawili ni kati ya bondia Fransic Miyeyusho na Fadhili Majiha  yote ikiwa ni mipambano ya raundi kumi kila moja

akizungumza mpambano huo promota Ally Mwazoa amesema ameamua kuwakutanisha mabondia hawo vijana ili wapate changamoto ya mchezo wa masumbwi na unapokuwa bondia unaitajika kila wakati uwe unacheza angalau kwa mwaka ucheze mara nne ili kiwango chako kiweze kupanda vinginevyo kama auchezi kiwango kinashuka hivyo nimeligundua hili na nimeamua kuwaletea mpambano huu mkali wa aina yake kwa ajili ya kuondoa ubishi

aliongeza kuwa siku hiyo kutakuwa na mipambano mingine ya utangulizi ambapo bondia Ramadhani Shauri atapambana na Saidi Mundi wa Tanga na Kazaula Pius wa Morogoro atakumbana na Mwinyi Mzengela wakati Shedrack Ignas atacheza na Husein Mbonde na Sadick Abdulazizi atakumbana na Godfrey Silve na Mohamed Amir atacheza na Fadhili Chamile

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali
na wengine wengi DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa mchezo huo. Rajabu Mhamila ‘Super D’, alisema kuwa kutakuwa na DVD ili kuweza kuwauzia mashabiki kwa ajili ya kujifunza Kanuni na Sheria za mchezo huo.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List