Na Chalila Kibuda, Dar
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhuongo, amejiuzulu wadhifa huo
kutokana na kuchoshwa na sakata la Akauti ya Tegeta Escrow.
Akizungumza
na waandishi wa habari Ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Barabara
ya Samora, Profesa Sospeter Muhongo amesema ameamua kujiuzulu ili kuwa
sehemu ya suluhisho la suala la akaunti ya Tegeta Escrow.
Aidha
Muhongo alisema kuwa suala la ankauti ya Tegeta Escrow limekuwa
likizungumzwa na kufanya mambo mengine yasiendelee na huku watanzania
walio wengi ni masikini wakihitaji umeme na sio kuuliza tegeta Escrow.
"Suala
hili mimi nililikuta toka mwaka 2012 na sijaweza kuchukua fedha katika
ankauti ya Tegeta Escrow, mimi sio mla rushwa, mimi sio mwizi na hakuna
mtu yeyote anayeweza kunipatia rushwa,
“Akaunti
ya Tegeta Escrow ilitawaliwa na mvutano wa kisiasa, kibiashara,
ubinafsi, uongozi na madaraka sasa watu wakae kujadili masuala mengine
hata bunge litumie muda kujadili mambo mengine pamoja na Chama cha
Mapinduzi (CCM) kinatumia muda mwingi kujadili suala la Escrow.
Hivyo
nimeamua kujiuzulu nafasi ya uwaziri ili niweze kuwa sehemu ya bunge na
kuendelea kuchangia katika masuala ya maendeleo kwani suala la escrow
sio suluhisho kwa watanzania". Alisema Muhongo
Muhongo
alisema kuwa anashukuru sana kwa kushirikiana vizuri na makamu wa Rais,
Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na baraza la mawaziri.
Aidha
alisema kuwa kuchelewa kujiuzulu alitaka wananchi wajiridhishe pamoja
na kumalizia kazi zingine ambazo zilikuwa mezani kwake ili zikamilike
hivyo asingeweza kufanya halaka kwani anajiamini kuwa ni mchapakazi na
muadilifu.
0 comments:
Chapisha Maoni