Mamilioni ya wapiga kura hii leo wanapiga kura nchini Nigeria kwenye uchaguzi ambao unaonekana kuwa wa kinyang'anyiro kikali tangu kumalizika kwa utawala wa kijeshi mwaka 1999.
Rais wa sasa Goodluck Jonathan anakabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa kiongozi wa zamani wa kijeshi Muhammadu Buhari ambaye alimshinda wakati wa uchaguzi wa urais miaka minne iliyopita.
Uchaguzi huo uliahirishwa kwa wiki sita kutokana na harakati za kundi la Boko Haram kaskazini mashariki mwa nchi.
Siku ya ijumaa jeshi la Nigeria lilisema kuwa liliharibu makao makuu ya Boko Haram kwenye mji mkuu wa Gwoza.
Mwandishi wa BBC anesema kuwa kuna hofu ya kutokea kwa mashambulio ya boko haram wakati wa uchaguzi .
0 comments:
Chapisha Maoni