WALEMAVU WA NGOZI LAZIMA WAPEWE UANGALIZI KWA JICHO LA TATU.

Hali ya majonzi bado imeendelea kutawala kwa walemavu wa ngozi,huku lawama zikiendelea kuelekezwa kwa serikali na jamii kwa kushindwa kupambana katika vita dhidi ya mauaji ya walemavu wa ngozi,yanayoendelea kutokea maeneo mbalimbali nchini.

Wananchi wanadai kuwa wauaji wanajulikana na jamii ila serikali imeshindwa kutengeneza mfumo mzuri wa kuwachukulia hukumu watuhumiwa na kuwalinda wanaotoa taarifa hizo.

Kijana Ashura mwanafunzi wa kidato cha nne mkoani Simiyu,analalamika kuwa bado wanahofu kutokana na ulinzi mdogo dhidi yao hasa nyakati za usiku

Viongozi wa dini pia wameona hali hii na udhaifu uliopo kati ya binadamu na hofu ya mungu.

Wanafunzi hawa kwa pamoja wanakutana kwenye kongamano la siku tatu la watoto walemavu jijini  Dar es salaam,ikijuimuisha watoto kutoka nchi za Sweden,Rwanda na Tanzania ambao ni mwenyeji,ili kujadili changamoto za kielimu.

Sweden,imepiga hatua kubwa katika kuwawezesha walemavu kuelimika ,na hapa watatoa uzoefu wao ili kuishawishi serikali ya Tanzania,kuiga mfano wake.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List