Mbunge wa Jimbo la Bahi mkoani Dodoma kwa tiketi ya CCM, Omary Badwel,
aliyekuwa akikabiliwa na mashtaka mawili ya kuomba na kupokea rushwa kwa
aliyekuwa Mkurugenzi wa Wilaya ya Mkuranga ameachiliwa huru na Hakimu
Mkazi Kisutu Hellen Riwa, baada ya upande wa mashtaka kushindwa
kuthibitisha shtaka dhidi ya mshtakiwa huyo.
Hakimu huyo alisema “katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haioneshi wazi kwamba mbunge huyo aliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha.”
Hakimu huyo alisema “katika ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka haioneshi wazi kwamba mbunge huyo aliomba na kupokea kiasi hicho cha fedha.”
"Kutokana na ushahidi wa upande wa mashtaka kushindwa kuithibitishia
mahakama pasipo shaka kwamba mbunge huyo ametenda makosa hayo, mshtakiwa
upo huru kuanzia sasa. HAta hivyo napenda kukuasa kuwa kama una
tofauti na watu katika jimbo lako kuwa makini na ujihadhari pamoja na
kujirekebisha kama una tabia ya kuombaomba jirekebishe na kuepuka kugusa
vitu vya watu," alisema hakimu.
0 comments:
Chapisha Maoni