SARAFU YA SH 500 YAUZWA KUTENGENEZEA MIKUFU YA FEDHA


Kuna taarifa kwamba watu wamekuwa wananunua sarafu mpya ya shilingi 500 kwa kiasi cha hadi Sh 2,500/= hadi sh 5,000/= na kisha kuiyeyusha kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha.
Hali hii imeelezewa kuwa ndio chanzo cha fedha hii iliyoingizwa kwenye mzunguko wa fedha kwa ajili ya kuchukua nafasi ya noti ya shilingi mia tano kuadimika mitaani kwa kiwango kikubwa.
Meneja Sarafu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Jovent Rushaka, amethibitisha kuwa Benki ina taarifa hizo na wanazifanyia kazi ili kufahamu sehemu zinakouzwa na wanaohusika. Aidha Meneja huyo amewaomba Watanzania wenye taarifa zozote kuhusiana na hujuma hizi atoe taarifa kwenye vyombo vya usalama.
Aidha Mkurugenzi wa Huduma za Kibenki BoT, Marcian Kobello amesema anashangazwa na hali ya watu kununua sarafu hiyo kwa ajili ya kutengenezea mikufu ya fedha kwani madini yaliyotumika kutengeneza sarafu hiyo ni chuma kwa asilimia 94 na nickel kwa asilimia 6; na amesisitiza kuwa hakuna kabisa madini ya fedha katika sarafu ya shilingi 500.
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List