ADC chama cha Wananchi wa Kawaida wapania kuleta Mabadiriko Tanzania

Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Said Miraji Abdullah akiongea na wananchi wa kijiji cha kwediboma Jana. 


  
Naibu katibu Mkuu wa Chma cha ADC bara Doyo Hasan Doyo akiongea na wananchi wa kijiji cha kwediboma Jana. 


Viongozi wa Chama cha ADC wakisubiri kugawa katiba inayopendekezwa kwa Wananchi

Chama cha Siasa ADC wapo ziara mkoani Tanga kuelezea sera za chama na kuhamasisha wananchi kujiandikisha katika daftari la kudumu la kupiga kura pamoja na kutoa Elimu juu ya katiba inayopendekezwa.
Chama hicho ambacho kina lengo la kufanya mmabadiriko kwa kutoa ushauri ndani ya Bunge pamoja na kuongea Sera zinazotekelezeka ili kuleta maendeleo kwa Tanzania..
Pia wametoa maoni ya kuhairisha mchakato wa kuipiga katiba mpya ili wananchi wapate nafasi ya kuisoma na kuijua vizuri.
ADC wametoa ushauri kura ya maoni ifanyike 2016 Baada ya uchaguzi mkuu unaotegemea kufanyika hivi karibuni.
Lengo lingine la ziara hiyo ni kuimarisha chama cha ADC kukijenga ili Umma UTAMBUE uwepo wake,kwa kuwafikia wananchi wa vijijini sambamba na kufanya maandalizi ya wagombea wa uchaguzi mkuu wa Udiwani,Ubunge na Urais.
Mwenyekiti wa Chama cha ADC Taifa Said Miraji Abdullah akiongea na wananchi wa kijiji cha kwediboma Jana amesema chama kipo kwa ajili ya wananchi na hawako Tayari kujiunga na Ukawa sababu ukawa upo kwa ajili ya manufaa ya watu binafsi.



Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List