BONDIA ADAM NGANGE WA CHANIKA AMSAMBALATISHA IDDI PIALALI WA BAGAMOYO

 Mabondia Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam kushoto  na Iddi Pialali wa Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakioneshana umwamba wa kutupiana makonde wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano huo wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWS
 Bondia Adam Ngange kushoto wa Chanika akimrushia konde la kulia bondia Iddi Pialala wa Bagamoyo wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika ukumbi wa chuo cha sanaa bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWS
Bondia Iddi Pialali wa Bagamoyo akimtupia makonde mfululizo bondia Adam Ngange wa Chanika wakati wa mpambano wao uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita  katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA Ngange alishinda kwa point mpambano uho wa raundi sita picha na SUPER D BOXING NEWS

Na Mwandishi Wetu
BONDIA Adam Ngange wa Chanika Dar es salaam amemsambalatika Iddi Pialali wa Kiwangwa Bagamoyo kwa point katika mpambano wao mkali wa raundi sita

uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha sanaa Bagamoyo TASUBA ambapo kulikuwa na shamla shamla za kutosha kwa upande wa Pialali

ukumbi ulifulika watu mbalimbali na mashabiki wa kutosha kabisa mpambambano ulivyo anza 

ngumi zilianza kupigwa kwa Pialali kwa kumshambulia sana Ngange mnamo raundi za mwanzo rakini kadri mpambano ulivyokuwa unasonga mbele na raundi kuzidi kwenda mbele

ndipo Ngange akazinduka na kuanza nae kumshambulia kwa kasi zaidi ambapo mpaka kufika raundi ya sita

raundi ambayo ilitawaliwa na ngange kupiga ngumi za misri ya paka anavyopiga kibao na kurudisha mkono alipo utoa mpaka raundi ya mwisho ya mchezo Ngange alikuwa mshindi kwa point mbili zaidi ya Pialali akika lilikuwa pambano zuri ambalo lilikusanya mashabiki wengi wa mkoa wa Pwani na Dar es salaam 

mpambano uho ulileta raha zaidi baada ya kudhuliwa na mabondia mbalimbali nchini wakiongozwa na Japhert Kaseba,Thomas Mashali. Said Mbelwa. Shabani Kaoneka na Ibrahimu Tamba mabondia ambao wanatamba kwa sasa nchini Tanzania
 
Share on Google Plus

About Unknown

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment

0 comments:

Inaendeshwa na Blogger.

Wanaofuata

TANGAZO

My Blog List